Seneta Yusuf Haji aendelea kupata nafuu

Seneta wa Garissa Yusuf Haji anaendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Agha Khan mjini Nairobi siku ya Jumanne.

Seneta huyo ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya usalama ya seneti alianguka akiwa nyumbani kwake mjini Garissa na kuvunjika mfupa ya nyonga.

Alisafirishwa kwa ndege hadi Nairobi kwa matibabu ya dharura na kufanyiwa upasuaji uliyochukuwa takriban saa tano.

Habari za kuumia kwake zilitangazwa na spika wa seneti Ken Lusaka.

Duru katika familia yake zilieleza meza yetu ya habari kwamba hali ya seneta huyo imeimarika na atatoka hospitalini punde tu madakatari wake watamruhusu kuondoka.

Haji pia ndiye mwenyekiti wa jopo maalum la BBI. Seneti ililazimika kuahirisha kikao cha Jumanne jioni baada ya kupokea habari za kuumia kwake.

Soma habari zaidi hapa;