Godwins Agut ambaye ni mkurugenzi wa shirika la Network Action Against Corruption alihusishwa katika Makala hiyo ya upekuzi iliyotayarishwa na NTV na kusimulia jinsi mabilioni ya kupambana na Covid 19 na misaada iliyotolewa na bwenyenye Jack Ma ilivyotumiwa vibaya .
Agutu alikamatwa pamoja na Alex Mutua na Ken Kimathi siu ya jumatano usiku . Watatu hao wanashtumiwa kwa kumteka nyara mkurugenzi wa Hi-tech Enterprise wakijifanya kuwa maafisa wa KRA na EACC kabla ya kuitisha hongo ya shilingi milioni 2 .
Mkuu wa DCI George Kinoti amesema watatu hao walikuwa wakishirikiana na watu wengine watatu ambao bado hawajakamatwa .
Watatu hao wanadaiwa kuwa wafanyikazi wa KRA waliotajwa kuwa ;Houdouvia Njoroge, Harrison Ochar na Brian Kimemia.
Walitumiwa magari mawili ya Prado yenye nambari za usajili GKB 070B na KCY 280Q na kuvamia afisi za mwathiriwa wao jijini Nairobi septemba tarehe 26 na kuichukua tarakilishi bebe yake .
" washukiwa hao walirejea tena septemba tarehe 29 na kuitisha shilingi milioni 2 kutoka kwa mwathiriwa na alipokosa kuzipata pesa hizo walimuingiza katika gari moja la GKB na kisha kumpeleka katika jumba la Lutheran Hse kwenye barabara Nyerere," Kinoti amesema
Kinoti ameongeza kwamba walimlazimisha mwathiriwa kuwapigia jamaa zake simu na walifaulu kukusanya shilingi nusu milioni na washukiwa wakaenda hadi nyumbani kwa mwathiriwa wao mtaani westland kuzichukua pesa hizo .
" Uchunguzi ulianzishwa na washukiwa wattau hao walikamatwa katika jumba la Lutheran House, huku ikigunduliwa kwamba nambari ya usajili ya gari walilotumia GKB 070B ni gari Land Rover Discovery ambalo linatumiwa na idara ya mahakama’ Kinoti amesema