Polisi walikuwa tayari wamepewa maagizo ya kuzuia mikutano ya Ruto

Jinsi serikali ilivyomzubaisha DP Ruto na Kusambaratisha ziara yake ya Kisii

Ruto hakujua serikali ilikuwa na nia ya kumzuia Kwenda Kisii na Nyamira

Muhtasari

 

  •  Ruto alilazimika kuahirisha hafla zake hadi wiki ijayo 
  •   Kanuni za kuandaliwa kwa mikutano ya hadhara zimeonekana kama njia ya kumthibiti Ruto 
  •  Wafuasi wa Ruto wamelalamikia hatua za polisi kuwazuia kukongamana 

 

Ufichuzi umetolewa jinsi serikali ilivyotumiwa uajanja kuhakikisha kwamba naibu wa rais William Ruto anakosa kuhudhuria half za hamrambee katika eneo la Kisii na Nyamira . Jumatano usiku Ruto alipokea mwaliko wa kuhudhuria mkutano wa baraza la mawaziri siku ifuatayo .

 Alitii na kuhudhuria mkutan huo  ambao uliongozwa na rais Uhuru Kenyatta .

  Mkutano huo ulijiri baada ya baraza la ushauri la usalama wa kitaifa kutoa mapendekezo ya kuzuia kampeini za mapema

 

Ruto  awali alikuwa amepanga kumaliza mkutano huo kufikia saa nne asubuhi kisha kusafiri kwa ndege hadi  Kebirigo huko Nyamira . Mkutano huo hata hivyo ulijikokota hadi saa sana mchana .

 Bila kujua kilichokuwa kikifanyika ,polisi walikuwa wamekusanywa ili kwenda kuwatawanya wafuasi wa Ruto waliokuwa wamemngoja Nyamira .

 Baadaye aligundua  kwamba  Polisi walikuwa wamekabiliana na wafuasi wake katika  maeneo ya Kitutu Msaba na Mugirango magharibi . Ilikuwa wazi kwamba serikali  ilikuwa imeshatekeleza mpango wa kuzuia mikutano yake .

 Naibu wa rais alilazimika kuchukua hatua ya haraka a baadaye akaamua kuahirisha hafla hizo . Ruto alipokuwa akikimbia kuhudhuria mkutano wa baraza la mawaziri , takriban viongozi 30 kutoka Kisii na Nyamira walikuwa Ikulu wakingoja kukutana na rais Uhuru

 Walikuwa wamepewa   mwaliko wa mkutano huo  siku iliyotanguliwa na waliongozwa na magavana  James Ongwae wa Kisii na JoHN  Nyangarama wa Nyamira .

 Kazi ya kuwatafuta wabunge hao na kuwapa mwaliko ilikabidhiwa mbunge wa Nakuru Ton west Samuel Arama .