DP Ruto aahirisha ziara yake ya Nyamira baada ya polisi kuwatawanya wafuasi wake kwa vitoa machozi

Muhtasari

 

  •  Ruto asema  mkutano huo sasa utaandaliwa alhamisi wiki ijayo
  • Awali polisi waliwatawanya wafuasi wake huko Nyamira 
  • Hayo yanajiri  siku moja baada ya baraza la ushauri la usalama wa kitaifa kutoa taarifa kali ya kukemea kampeini za kisiasa wakati huu

 

 

 Naibu wa rais William Ruto ameahirisha ziara yake ya kwenda Nyamira baada ya polisi kuwatawanya wafuasi wake kutumia vitoa machozi

  Ruto ametumia twitter kuwashambulia polisi kwa kuvuruga mkutano wa Amani . amesema baada ya kushauriana na wabunge  Kemosi, Mose,Nyamoko,  chama cha boda boda na viongozi wa makanisa waliokuwa wamemualika huko Nyamira mkutano huo sasa utafanyika alhamisi wiki ijayo.

 

 Amesema polisi hawafai kuvuruga mkutano unaolenga kuwahamasisha kiuchumi wakenya

 Awali polisi  katika kaunti ya Nyamira waliwaamrisha wananchi kutoka katika uwanja wa shule ya upili ya Keberigo ambako mkutano mmoja wa Ruto ulitarajiwa kufanywa .

 Polisi walifika katika uwanja huo na kuitaka bendi ya muziki iliyokuwa ikiendelea na kuwatumbuiza wananchi kuondoka  wakisema hakuna mkutano ambao ungefanyika katika shule hiyo .

 Tayari kundi la Ruto lilikuwa limeshafika katika maeneo yote ya mikutano yake kabla ya kuwasili kwake  kwa sabau alikuwa amehudhuria mkutano wa baraza la mawaziri Nairobi .

 Tulizungumza wiki jana na kamishna wa kaunti kuhusu mkutano wetu na akakubali ,sasa kwa bahati mbaya ameamua kuuvurug’ amesema mbunge Kemosi