'Ninaweza pewa mtu mwingine lakini si kama pendo,'Mama Pendo azungumza katika uzinduzi wa BBI

Muhtasari
  • Wacha damu ya mwanagu Pendo iwe ya mwisho,baba yake Pendo azungumza wakati wa uzinduzi wa BBI
  • maua yaling'olewa kutoka bustani yangu na hayawezi kubadilishwa mama pendo azungumza
  • Baby Pendo aliua mnamo mwaka wa 2017 na polisi

Maua yaling'olewa kutoka bustani yangu na hayawezi kubadilishwa ni matamshi yake Mama pendo ambayo aliyasema wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa BBI.

Mtoto Pendo aliuawa na polisi mnamo mwaka wa 2017,Agosti,11, baada ya mahakama ya juu kubatilisha uchaguzi wa urais.

"Maua yaling'olewa kutoka bustani yangu na hayawezi kubadilishwa, ninaweza pewa mtu mwingiine lakini si kama pendo

 

Naomba wanasiasa ikue mwisho wa kile kilitendeka mwwaka wa 2017,wanasiasa ambao wanashindwa katika uchaguzi wanapaswa kukubali matokeo

Hata kwa ripoti ya BBI tunapaswa kujisomea natuweze kupiga kura ya ndio au la tunavyoona inafaa." Alisema Mama Pendo.

Mama huyo aliwauliza wanasiasa kuchunga  maneno yanotoka katika ndimi zao ili zisiweze kuleta vurugu miongoni mwa wananchi.

Unapokuja chunga vitu zinatoka kwa ndimi zenu. Msifanye tupigane halafu wewe unasonga mbele na maisha yako." Alizungumza.

Baba Pendo bwana Joseph Abanta alipopewa fursa ya kuzungumza aliwahimiza wakenya wasiweze kudanganywa na wanasiasa.

"Wakenya sisi ni watu wazuri,wacha tusidanganywe na siasa wacha damu ya mwanangu iwe ya mwisho kumwagika kwa ajili ya wanasiasa

Naomba Rais Uhuru vile mumeshikana na Raila Odinga msiachane mkono. Naona BBI italeta mabadiliko kwa maisha yetu.

 

Rais kumbuka familia ya Baby Pendo msituache hivo. Mumetuacha tunateseka." Alizungumza.