DCI George Kinoti kuhukumiwa kwa kutotii maagizo ya mahakama

Muhtasari
  • DCI Kinoti kuenda mbele ya mahakama mnamo tarehe 24 Novemba
  • Kinoti anahukumiwa kwa kupuuzilia mbali maagizo ya korti
George Kinoti
Image: maktaba

Mkurugenzi wa Idara ya Kuchunguza Uhalifu (DCI), George Kinoti ameamuriwa kufika mbele ya mahakama kuhukumiwa kwa madai ya kutotii maagizo ya korti.

Jaji Janet Mulwa alisema Kinoti ana hatia ya kupuuza amri ya mahakama mnamo Julai 29, wakati mahakama hiyo iliamuru idara yake kuachilia malori mawili yaliyokamatwa miaka miwili iliyopita kwa madai ya kusafirisha sukari ghushi iliyokuwa na chembechembe za zebaki.

Kinoti anatarajiwa kufika mbele ya Mahakama ya Kerugoya mnamo Novemba 24 kuhukumiwa

Hii si mara ya kwanza Kinoti kujipata taabani na Idara ya Mahakama kwa kupuuza amri ya korti.

Mnamo tarehe 2 Mei 2020 KInoti aliamuriwa na korti kuachilia malori hayo yaliokuwa katika afisi za DCI Nairobi ilhali hakuweza kufanya hivo.

Mwanabiashara Njiru kupitia kwa wakili wake Brian Khaemba alisema kwamba KInoti aliamurishwa na mahakama kumlipa shillingi 90,000 na kuachilia malori hayo ilhali hakuweza kufuata maagizo ya korti.