'Nilipatikana na Corona wiki tatu zilizopita,' Mbunge Nixon Korir afunguka

Mbunge wa Langata Nixon Korir amefunguka kuhusu hali yake ya Covid-19 status baada ya ripoti kuwa alikuwa amelazwa Nairobi hospital akiugua virusi hivyo.

Mbunge huyo wa Jubilee akizungumza na The Star alifichua kuwa alipatikana na virusi hivyo wiki tatu zilizopita na amekuwa akiugulia nyumbani.

“Nilipatikana na Covid-19 wiki tatu zilizopita lakini nimekuwa nikijitenga, Nitafanyiwa vipimo hapo kesho (Jumapili). Korir aliambia gazeti la The Star kupitia mahojiano ya simu.

Mjumbe huyo kijana alisema kuwa pindi tu alipopatikana na virusi hivyo alikimbilia hospitali moja ya Nairobi ambapo alitibiwa na akuachiliwa akaugulie nyumbani.

Alifichua kuwa alipata dalili za ugonjwa huo mapema na akakosa hewa ya kutosha lakini madaktari walimshukulia na kuimarisha hali yake.

Alikana madai kuwa bado amelazwa hospitalini huku hali yake ikiwa mbaya.

“Nimekuwa nikiugulia nyumbani. Wanaosema kuwa nimelazwa hospitalini ni waandishi wa habari tu wanaosema chenye wanachotaka kusema.,” alisema.

Mbunge huyo anatarajiwa kufanyiwa vipimo vingine hii leo baada ya dalili alizokuwa nazo kuisha.

“Natumai kurudi kazini wiki ijayo. Kila kila kiko sawa sahii." Korir alisema huku akiwa na wingi wa matumaini.

Korir, ambaye ni rafikiye wa naibu wa rais William Ruto ameongeza kwa idadi ya wabunge walioambukizwa virusi hivyo tangia kisa cha kwanza cha Corona kuripotiwa nchini.