'Tuombee familia yake,'Waziri Fred Matiang'i amuomboleza gavana Nyagarama

Waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang'i akiomboleza kifo chake gavana wa kaunti ya Nyamira Nyagarama alisema kwamba serikali itajpanga na kutangaza siku ya mazishi ya mwendazake.

Nyagarama alipelekwa hospitalini wiki tatu zilizopita baada ya kupatikana na virusi vya corona.

Aliwekwa katika msaada wa maisha jumapili, ambapo jumatatu familia yake ilipigiwa simu baada ya hali yake ya afya kuzidi kudhoofika.

 

"...Alikuwa akijihisi vibayakwa muda  na wanawe wote wako hapa, ndio tumefika hapa kama serikali tutajipanga na kuona tutakalo lifanya

Ni huzuni mwingi, Nyagarama alikuwa mtu mzuri na alikuwa baba na mzee wa kila mtu." Matiang'i alizungumza hayo akiwa katika makafani ya kuhifadhi maiti ya Lee.

Huku akimuomboleza mwendaazake Matiang'i alisema kwamba gavana huyo alikuwa mtulivu na ambaye alitaka sana umoja wa taifa.

"Wacha tukae pamoja, na tuombee familia ya mwendazake ili Mungu awape nguvu ." Alisema Matiang'i.

Gavana huyo aliaga huku akiwa na miaka 74.