Buriani: CS Matiang'i na Raila Odinga wawaongoza waombolezaji kumpa Nyagarama heshima za mwisho

Muhtasari
  • CS Matiang'i na Raila Odinga wawaongoza waombolezaji kumpa Nyagarama heshima za mwisho
  • Nyagarama aliaga dunia ijumaa iliyopita kutokana na virusi vya corona

Waziri wa mambo ya ndani Fred Matiangi na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga amewaongoza familia, marafiki, viongozi na waombolezaji katika kaunti ya Nyamrira kumpa Gavana Nyagarama heshima zake za mwisho.

Nyagarama aliaga dunia ijumaa 18 Desemba mwaka huu.

Viongozi na waombolezaji walikusanyika katika shule ya msingi ya Nyamira kupa mwendazake heshima za mwisho.

Viongozi walihudhuria mazishi hayo ni pamoja na jaji mkuu David Maraga, magavana walikuwa

Wycliffe Oparanya (Kakamega), Anyang' Nyong'o (Kisumu), James Ongwae (Kisii), Cyprian Awiti (Homa Bay), Okoth Obado (Migori), Wilbur Otchillo (Vihiga), Hillary Barchok (Bomet) and Cornel Rasanga (Siaya) miongoni mwa wengine.

Pia wabunge walihudhuria hafa hiyo huku wakiwa wameongozwa na Vincent Kemosi wa wadi ya mugirago.

Rais Uhuru Kenyatta alitarajiwa kuongoza hafla iyo lakini badala yake alimtuma waziri Matiang'i.