Safari yetu ya kufanya kenya bora haizuiliki-gavana Charity Ngilu

Muhtasari
  • Gavana wa Kitui Mama Charity Ngilu amesisitiza kuwa azma ya kuwa na Kenya bora haiwezi kuzuilika

Gavana wa Kitui Mama Charity Ngilu amesisitiza kuwa azma ya kuwa na Kenya bora haiwezi kuzuilika.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter, Ngilu ambaye ni mmoja wa magavana wanawake waanzilishi nchini Kenya alisema kuwa ilikuwa tu baada ya ugatuzi ndipo watu wa kaunti yake (Kitui) walianza kufaidika na Kenya huru.

Gavana huyo aliendelea na kusema kuwa ni ugatuzi tu itawezesha Kenya kufikia usawa wa kikanda, na  anaamini  hayo pamoja na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga.

 

“Ni baada ya ugatuzi tu kwamba watu wa Kaunti ya Kitui walianza kufaidi matunda ya Kenya huru

Kupitia Ugatuzi tu ndio maeneo yote ya Kenya yatapata usawa. Kama vile mimi na @RailaOdinga tunaamini, safari yetu ya  kufanya Kenya bora haiwezi kuzuilika !! ” Aliandika Ngilu.

Ngilu amekuwa katika mstari wa mbele huku akipigia debe muswada wa maradiano na ripoi ya BBI.