Wanawake 2 wakamatwa kwa jaribio la udanganyifu Mwea Mashariki

Muhtasari
  • DCI yawakamata wanawake 2 kwa jaribio la udanganyifu mwea mashariki

Wapelelezi wa DCI Jumatatu waliwakamata wanawake wawili kwa madai ya kupumbaza na kujaribu kumwibia mwanamume huko Mwea Mashariki.

Grace Njeri na Evelyne Esendi wenye umri wa miaka 29 na 32 wanashukiwa kuwekea chumba katika nyumba ya wageni ya Village Inn huko Mwea Mashariki Jumapili na kumshawishi mwathiriwa wao Daniel Gathege Maira kwa mtego wao.

DCI alisema katika taarifa kupitia Twitter kwamba wawili hao walionekana wakitoka kwenye chumba hicho na kuenda katika eneo la ATM, ambapo wapelelezi wanaamini shughuli zingine zilifanywa.

"Ni hatua hii ya tuhuma ambayo ilivutia mdhibiti wa CCTV huko Nice Digital City, ambaye mara moja aliwaonya Maafisa wa Polisi walio katika kituo cha Polisi cha Wanguru.," Kurugenzi hiyo ilisema.

Baada ya uchunguzi zaidi, wahusika wa DCI walimkuta mWANAMUME huyo akiwa amelala kitandani akiwa hajitambui.

Alikimbizwa katika Hospitali ya Misheni ya Comrade ambapo sasa anapokea matibabu.

"Kama mwathiriwa anaendelea kupona, washukiwa wawili wanasalia kizuizini kujibu mashtaka ya udanganyifu," DCI alisema.