Covid-19:Watu 1,441 wapona corona huku 21 wakiaga dunia

Muhtasari
  • Watu 1,441 wapona corona huku 21 wakiaga dunia
  • Watu 965 wapatikana na virusi vya corona Kati ya Maambukizi hayo mapya 907 ni wakenya huku 58 wakiwa ni raia wa kigeni

Watu 965 wamepatikana na virusi vya corona na kufikisha idadi jumla ya 153,488 ya watu waliopatikana na corona ,hii ni kutokana na sampuli 7,311 zilizopimwa chini ya saa 24.

Kati ya Maambukizi hayo mapya 907 ni wakenya huku 58 wakiwa ni raia wa kigeni.

Pia 560 ni wanaume huku 405 wakiwa ni wanawake, mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 3 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 101

 
 

Watu 1,441 wamepona maradhi hayo na kufikisha idadi jumla ya 105,279 watu waliopona corona.

Vile vile watu 21 wamepoteza maisha yao kutokana na corona na kufikisha idadi jumla ya 2,540ya watu walioga dunia kutokana na corona.

Wagonjwa 1,509 wamelazwa hospitali tofauti humu nchini huku 6,808 wakipokea matibabu wakiwa wamejitenga nyumbani.

Wagonjwa 240 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).