Raila Odinga atembelea wajane wa John Magufuli na Benjamin Mkapa Janet na Anna

Muhtasari
  • Raila Odinga atembelea wajane wa John Magufuli na Benjamin Mkapa Janet na Anna
Image: Raila Odinga/Twitter

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga siku ya JUmatano aliwatembelea wajane wa John Magufuli na Benjamin Mkapa Janet na Anna.

Haya yanajiri baada ya kutoka Zambia kwa hafla ya kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo Hakainde Hichilema.

Raila likuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri wa Kiafrika walioandaa sherehe za kuapishwa kwa rais mpya.

Akiwa Dar es Salaam, alijishughulisha na familia mbili ambazo hivi karibuni zilipoteza wazee wao.

"Nilipita kutembelea familia za Marais wa rafiki yangu Benjamin Mkapa na John Magufuli. Nimefurahi kuwaona Mama Anna Mkapa na Mama Janeth Magufuli wakiwa na roho nzuri. Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi," alisema Raila.

Magufuli alikufa Machi 17, 2021, kulingana na tangazo lililotolewa kwenye runinga ya serikali na Makamu wa Rais wa wakati huo Samia Suluhu.

Mkapa alikufa mnamo Julai 2020 baada ya kupigana na ugonjwa ambao haukufahamika.

Marehemu Magufuli alikuwa ametangaza kifo hicho wakati wa hotuba kwa njia ya televisheni.