IPOA yaanzisha uchunguzi baada ya polisi kuua watu 6 kabla ya kujiua

Muhtasari
  • Aliwataka maafisa wa polisi kuchunguza kikamilifu mbinu za kushughulikia masuala yanayoathiri kazi yao
Image: Enos Teche

Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi inachunguza kisa ambapo afisa wa polisi alimuua mkewe na wengine sita kabla ya kujitoa uhai katika eneo la Kabete, Nairobi.

".. Mamlaka leo asubuhi ilituma timu yake ya Majibu ya Haraka kupata habari ambazo zinaweza kuwa muhimu katika kufichua mazingira yanayozunguka tukio la ufyatuaji risasi," mwenyekiti Anne Makori alisema.

"Baada ya kukamilika kwa uchunguzi, Mamlaka itatoa mapendekezo sahihi kwa taasisi zinazohusika."

Aliwataka maafisa wa polisi kuchunguza kikamilifu mbinu za kushughulikia masuala yanayoathiri kazi yao.

Hii inajumuisha kuwasilisha malalamiko kwa Ipoa kupitia nambari ya bila malipo 1559 kando na kutumia mara kwa mara huduma za ushauri nasaha zinazotolewa na Tume ya Kitaifa ya Huduma ya Polisi.

"Ipoa inasalia kujitolea kuwa huru, bila upendeleo na haki," alisema.

Waliofariki ni pamoja na mkewe, majirani na waendesha bodaboda ambao walikuwa wamekimbilia nyumbani kwake kuangalia kilichojiri waliposikia milio ya risasi Jumanne asubuhi.

Polisi walisema konstebo Benson Imbatu aliye katika kituo cha polisi cha Kabete alienda nyumbani akiwa na bunduki yake aina ya AK47 na kuzua ugomvi na mkewe Carol Imbatu.