Susan Kihika akosolewa kufuatia matamshi makali dhidi ya Raila Odinga

Muhtasari

•Mwandani huyo wa naibu  Rais William Ruto akizungumza  alisema wazi wamechoka na historia ambayo imekuwa ikitajwa kila wakati.

•Mdahalo mkubwa ulizuka katika mtandao wa Twitter baadhi ya Wanamitandao wakimkumbusha Kihika historia yake.

Seneta wa Nakuru Susan Kihika
Image: Hisani

Seneta wa Nakuru Susan kihika amejiipata pabaya kosolewa kufuatia maneno aliyotoa kuhusu kinara wa ODM Raila Odinga.

Mwandani huyo wa naibu  Rais William Ruto akizungumza  alisema wazi wamechoka na historia ambayo imekuwa ikitajwa kila wakati ilhali hakuna anayesema vile nchi itakuwa katika siku za usoni

“Tumesikia  sana kuna wengi wametembea na kila wakati wakipewa kipaza sauti hawatwambii chenye watafanya tukiendelea mbele, wanatwambia mambo ya zamani, wamekwama kwa historia”

Maneno haya hayakuchukuliwa rahisi na baadhi ya wakenya ambao walieleza ghadhabu yao kupitia mitandao ya kijamii.

Mdahalo mkubwa ulizuka katika mtandao wa Twitter baadhi ya Wanamitandao wakimkumbusha Kihika historia yake.

@Airo Nick “wale hawajui historia Baba anawakumbusha”

@Brigade Ole  “Kama unasimama lazima tujue historia. Afadhali tuchague shetani tunamjua kuliko malaika hatumjui”

Susan ambaye anamezea kiti cha ugavana kaunti ya Nakuru kiti  kinachokaliwa na Lee kinyanjui amekuwa akiendesha kampeni  moto katika ngome hiyo inayokisiwa kuwa na waungaji mkono wengi wa mrengo wa UDA.

 Kihika hajawasaza wanaomkosoa mitandaoni huku akiwajibu kupitia mtandao wake wa twitter.