PSC imekanusha kumteua Jacque Maribe kama Mkuu wa Mawasiliano katika Wizara ya Utumishi wa Umma

Katika taarifa Machi 14 Alhamisi, mwenyekiti wa PSC Anthony Muchiri alisisitiza kuwa hakuna uteuzi kama huo ambao umefanywa na bodi haijapokea ombi lolote la kuajiri Maribe.

Muhtasari
  • "Kwa rekodi, nafasi iliyotajwa itajazwa kupitia mchakato wa kuajiri wenye ushindani iwapo nafasi itatokea," alisema Muchiri.
Jaque Maribe
Image: Instagram

Tume ya Utumishi wa Umma (PSC) imepuuzilia mbali ripoti kwamba wamemteua aliyekuwa mwanahabari Jacque Maribe katika Wizara ya Utumishi wa Umma, Utendaji na Usimamizi wa Uwasilishaji kuwa Mkuu wa Mawasiliano.

Katika taarifa Machi 14 Alhamisi, mwenyekiti wa PSC Anthony Muchiri alisisitiza kuwa hakuna uteuzi kama huo ambao umefanywa na bodi haijapokea ombi lolote la kuajiri Maribe.

"Kwa rekodi, nafasi iliyotajwa itajazwa kupitia mchakato wa kuajiri wenye ushindani iwapo nafasi itatokea," alisema Muchiri.

Haya yanajiri wiki moja baada ya ripoti kadhaa kuthibitisha kwamba Maribe alipata kazi hiyo ya pesa nyingi, iliyokuja siku chache baada ya kuachiliwa katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani mnamo 2018.

Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Utumishi wa Umma (CS) Moses Kuria hata alinukuliwa na chombo kimoja cha habari kikithibitisha uteuzi huo.

“Ni kweli ila si mimi niliyemteua bali Tume ya Utumishi wa Umma,” alisema Kuria.

Akitumia mitandao yake ya kijamii mnamo Machi 10, Mtaalamu wa Mikakati wa Kidijitali Dennis Itumbi alimshukuru CS Kuria kwa uteuzi huo.

"Hongera, Jacque Maribe. Mungu akubariki unapohudumu," Itumbi aliandika.

"Asante Moses Kuria kwa kusimama na kizazi, tafadhali endelea kufanya vyema na kunyoosha mkono wako," mwanamkakati huyo aliongeza.