Polycap Igathe kupeperusha bendera ya Azimio la Umoja - One Kenya Nairobi

Muhtasari

Hatimaye Polycap Igathe ametangazwa kuwa mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Nairobi kupitia tikiti ya muungana wa Azimio la Umoja - One Kenya.

Hatimaye Polycap Igathe ametangazwa kuwa mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Nairobi kupitia tikiti ya muungana wa Azimio la Umoja - One Kenya.

Taarifa hiyo imetangazwa na kinara wa ODM, Raila Odinga katika jumba la KICC ambapo viongozi hao walikuwa wakifanya mkutano wao ili kumtafuta mgombea.

Philip Kaloki wa Wiper sasa atakuwa mgombea mwenza wa Igathe katika kinyang'anyiro hicho cha Agosti 9.

Mbunge wa Westlands, Tim Wanyonyi ambaye pia alikuwa ameonyesha azma ya kuwania wadhfa huo sasa amesitisha azma yake na badala yake kuamua kuwania awamu nyingine ya kiti cha ubunge katika eneo bunge la Westlands.

Aidha, katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna atawania kiti cha Useneta kupitia tikiti ya muungano wa Azimio.

Esther Passaris naye atakuwa mgombea wa kiti cha uwakilishi wanawake katika uchaguzi mkuu ujao.

Richard Ngatia ambaye pia alikuwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo sasa atajukumika kama mjumbe maalum wa biashara katika serikali ya rais Uhuru Kenyatta, huku uteuzi wake ukitekelezwa mara moja.