"Marufuku kushiriki maandamano kaunti ya Kisumu" - Gavana Anyang' Nyong'o atangaza

Nyong'o alisema kwambac hatua hiyo ni kudumisha amani na usalama Kisumu na kutoa fursa kwao kujiunga na maandamano Nairobi.

Muhtasari

• Nyong’o aliwataka wakaazi wa mji huo wa tatu kwa ukubwa Kenya kushirikiana kwa ukaribu na maafisa wa polisi ili kudumisha Amani na usalama katika kaunti hiyo.

Gavana Nyong'o apiga marufuku Kisumu.
Gavana Nyong'o apiga marufuku Kisumu.
Image: Facebook

Gavana wa kaunti ya Kisumu profesa Anyang Nyong’o ametangaza amrufuku ya mikusanyiko yoyote ya maandamano katika kaunti hiyo kuelekea Alhamisi siku ya maandamano.

Kupitia barua iliyotiwa saini na gavana huyo, maandamano hayo yalipigwa marufuku kutoka kaunti hiyo kwa kile alisema kwamba ni hatua inayonuiwa katika kujiunga na wenzao kuendeleza maandamano nje ya kaunti hiyo – haswa haswa kaunti ya Nairobi.

“Baada ya mashauriano ya muda na viongozi wa Azimio la Umoja One Kenya, tumefikia uamuzi kwamba maandamano yote ndani ya Kisumu yamesitishwa kuanzia leo ili kutoa nafasi kwetu kujiunga na maandamano Nairobi,” sehemu ya barua hiyo ilisema.

Nyong’o aliwataka wakaazi wa mji huo wa tatu kwa ukubwa Kenya kushirikiana kwa ukaribu na maafisa wa polisi ili kudumisha Amani na usalama katika kaunti hiyo.

Nyong’o alisema kwamba wapiga kura wake wamekuwa waadilifu katika kuitikia wito wa kinara wa ODM Raila Odinga katika kufanya maandamano yanayolenga kushinikiza serikali ya Kenya Kwanza kupunguzac gharama ya maisha, uteuzi alioutaja kama usio halali wa makamishna wapya wa IEBC miongoni mwa matakwa mengine, jambo ambalo alisema litaendelea hata ingawa si ndani ya kaunti hiyo ya Ziwa Victoria.