Mkewe mbunge wa Kapenguria Samuel Muroto ameaga dunia

Moroto alielezea msiba huo kuwa ni mgumu kwa familia hiyo licha ya wao kukubaliana na hali halisi.

Muhtasari

• "Licha ya jitihada zetu za kumwokoa, Mungu amechagua kumpa pumziko la milele."

• Moroto alielezea msiba huo kuwa ni mgumu kwa familia hiyo licha ya wao kukubaliana na hali halisi.

MKEWE MBUNGE WA KAPENGURIA
MKEWE MBUNGE WA KAPENGURIA
Image: HISANI

Mbunge wa Kapenguria Samuel Moroto yuko katika majonzi kufuatia msiba wa mkewe.

Inasemekana Mary Muroto alikata roho siku ya Ijumaa.

Mbunge huyo katika taarifa yake kuhusu kifo chake alifichua kuwa mke alifariki kutokana na saratani.

"Ni kwa mioyo mizito kwamba tunashiriki habari za kuaga kwa mke wangu mpendwa, Mary Saisy Moroto. Vita vyake vya ujasiri dhidi ya saratani, adui aliyesababisha maumivu yasiyofikirika, vimefikia kikomo," mbunge huyo alifichua.

"Licha ya jitihada zetu za kumwokoa, Mungu amechagua kumpa pumziko la milele."

Moroto alielezea msiba huo kuwa ni mgumu kwa familia hiyo licha ya wao kukubaliana na hali halisi.

"Kukubaliana na kuondoka kwake ni changamoto kubwa, na ukweli wa kutokuwepo kwake bado ni mgumu kufahamu. Tunapata faraja katika kumbukumbu za nguvu zake, upendo, na nyakati zisizohesabika tulizoshiriki," alisema.

Gavana wa Pokot Magharibi Simon Kachapin pia aliomboleza kifo cha mke wa mbunge huyo akimtaja kama mama mwenye upendo aliyeacha urithi mzuri kwa wengi waliotangamana naye.

“Hadi kifo chake, marehemu Mama Cherop alisalia kuwa mama mwenye upendo na kujitolea, na kuacha alama ya kukumbukwa mioyoni mwa waliomfahamu,” gavana huyo alibainisha.

"Pole zangu za dhati kwa Mhe. Moroto, familia yake na marafiki. Kumbukumbu nzuri na upendo alioshiriki Mama Cherop, zilete faraja na faraja katika kipindi hiki kigumu."