Tanzia! Amos Kimunya afiwa na mkewe, amuomboleza kihisia

Aliyekuwa mbunge wa Kipipiri Dkt Amos Kimunya ameomboleza kifo cha mkewe Lucy Kimunya.

Muhtasari

•Katika taarifa yake, kiongozi huyo wa zamani wa wengi bungeni alitangaza kwamba mkewe alifariki usiku wa kuamkia Jumanne.

“Nenda sawa mpendwa wetu Lucy, tutakukumbuka sana. Mawasiliano zaidi yatafuata," Bw Kimunya aliomboleza

Marehemu Lucy Kimunya
Image: FACEBOOK// DR AMOS KIMUNYA

Aliyekuwa mbunge wa Kipipiri Dkt Amos Kimunya ameomboleza kifo cha mkewe Lucy Kimunya.

Katika taarifa yake ya kihisia siku ya Jumanne, kiongozi huyo wa zamani wa wengi bungeni alitangaza kuwa mkewe alifariki usiku wa kuamkia Jumanne.

Kimunya alifichua kuwa marehemu Lucy alikuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Nairobi alipokata roho.

"Ni kwa huzuni kubwa na kukubali kwa unyenyekevu mapenzi ya Mungu kwamba ningependa kutangaza kwamba Jumanne hii asubuhi saa tisa asubuhi mke wangu mpendwa Lucy alienda kuwa na bwana, alipokuwa akipokea huduma katika Hospitali ya Nairobi," Amos Kimunya alitangaza kupitia mtandao wa Facebook.

Mwanasiasa huyo aliendelea kuzungumzia nafasi kubwa ambayo marehemu alicheza katika maisha yake na jamii kwa ujumla.

"Alikuwa nguzo muhimu katika maisha yangu ya kibinafsi na ya kisiasa, alichangia pakubwa kuifanya jamii yetu kuwa ya kijani kibichi kupitia mipango mbalimbali na kuunga mkono vijana na wanawake," alisema.

Aliongeza, “Nenda sawa mpendwa wetu Lucy, tutakukumbuka sana. Mawasiliano zaidi yatafuata."

Makumi ya Wakenya walimiminika kumfariji Bw Kimunya na familia yake huku wakimuomboleza mpendwa wao.

Soma jumbe za faraja kutoka kwa baadhi ya Wakenya wa Facebook:

Hon Isaac Kung’u Wanjiru: My sincere condolences. We will remember Madam Lucy as a great proponent of environment conservation.May her soul rest in eternal peace.

Martin Mungai: Hon.Dr. Amos Kimunya , so sorry for this big loss. Our prayers and thoughts are with you as you go through this difficult period of the loss of your dear wife. It is well sir.

Anthony Methu: Very Sad news. Condolences to the family. May her soul RIP.

Abel Leo Mosiah; May you receive the comfort you deserve as a bereaved family.

Wanjiku Muhoho: My condolences to you and your entire family. May the Lord rest her soul in eternal peace.