Ukraine yasema wanajeshi 3,500 wa Urusi wameuawa kufikia sasa

Muhtasari

•Wanaongeza kuwa Urusi pia imepoteza ndege 14, helikopta 8, na mizinga 102 hadi sasa. 

Image: REUTERS

Jeshi la Ukraine limechapisha kile wanachodai kuwa ni mwanzo wa hasara ya Urusi.

Kulingana na chapisho kwenye ukurasa wake wa Facebook, zaidi ya wanajeshi 3,500 wa Urusi waliohusika katika uvamizi huo wameuawa na karibu 200 kuchukuliwa wafungwa.

Wanaongeza kuwa Urusi pia imepoteza ndege 14, helikopta 8, na mizinga 102 hadi sasa. BBC haiwezi kuthibitisha kwa uhuru madai yoyote kati ya haya.

Urusi hadi sasa haijatambua majeruhi wowote.

Zelensky achapisha video, akanusha kuwa ametoa wito wa kujisalimisha

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amechapisha video aliojipiga mwenyewe kwenye Twitter akitembea katika mitaa ya Kyiv katika juhudi zinazoonekana kupambana na uvumi kwamba amelitaka jeshi kujisalimisha kwa wanajeshi wa Urusi.

"Kuna habari nyingi za uwongo mtandaoni ambazo ninatoa wito kwa jeshi letu kuweka silaha chini, na kwamba kuna usafirishaji wa kuwaondoa watu," alisema akiwa nyuma ya Jumba la Gorodetsky la Kyiv.

"Niko hapa. Hatutaweka chini silaha zetu. Tutatetea taifa letu."