Ukraine yafungua simu ya dharura kwa Waafrika wanaokimbia vita

Muhtasari
  • Ukraine yafungua simu ya dharura kwa Waafrika wanaokimbia vita
Image: BBC

Serikali ya Ukraine imeanzisha simu ya dharura kwa Waafrika na raia wa Asia wanaokimbia uvamizi wa Urusi, kulingana na waziri wa mambo ya nje.

Hatua hii inakuja kufuatia madai yaliyoenea ya ubaguzi wa rangi yanayowakabili waafrika wanaojaribu kuondoka nchini humo.

Wanafunzi wengi kutoka Afrika nchini Ukraine wameshirikisha simulizi za wao kuzuiwa na afisa wa usalama wa Ukraine kuondoka nchini humo.

Katika ujumbe wake wa Twitter, Waziri wa Mambo ya nje Dmytro Kuleba alisema mamlaka "zinafanya kazi kwa bidii" kuhakikisha usalama na kupita kwa wanafunzi wa Kiafrika na Asia.

Wakazi wa Kyiv bado wamejificha katika handaki

Wakazi wa Kyiv wa rika zote - watu wazima na watoto - walielekea tena chini ya ardhi jana usiku wakati mji mkuu ukiendelea kulengwa.

Baadhi, kama inavyoonyeshwa hapa, walishuka hadi kwenye vituo vya metro ambavyo vinatumika kama makazi.

Kiasi cha watu 15,000 wanajihifadhi katika vituo hivyo, meya wa jiji hilo amekadiria.

BBC correspondents have said the blasts could be heard from two storeys underground in their bunker.

Baadhi walifanikiwa kulala huku wengine wakijaribu kuwaburudisha watoto wadogo.

Milipuko minne mikubwa ilisikika usiku kucha na kunaswa kwenye video na mashahidi, ingawa haijabainika malengo yalikuwa nini au kama kulikuwa na vifo.

Waandishi wa BBC wamesema milipuko hiyo inaweza kusikika kutoka ghorofa mbili chini ya ardhi katika chumba chao cha kulala.