(Video) Watoto 5 wa familia moja waliokufa kwa kulishwa chakula chenye sumu wazikwa

Watoto hao watano wa kutokqa familia moja walifariki mmoja baada ya mwingine chini ya wiki moja

Muhtasari

• Kabla ya kufa, kila mmoja alikuwa akiteta maumivu makali ya tumbo na gesi kujaa kabla ya kukata roho.

• Mpaka wakati wa maziko yao, wqazazi wao tayari walikuwa wameshikiliwa kama washukiwa wakuu.

Kwa wiki mbili sasa mamlaka nchini Tanzania zimekuwa zikitangaza vifo kutokana na ugonjwa usiojulikana ambao unasemekana ni kutokwa damu puani.

Katika jimbo la Arusha, kaskazini mwa taifa hilo, familia moja inazidi kuomboleza vifo vya wanao watano chini ya wiki moja ambao wote wanasemekana kufariki kutokana na maumivu ya tumbo.

Vifo hivyo vimetokea katika Kijiji cha Mswakini wilayani Monduli, Mkoa Arusha nchini Tanzania na wote kabla ya kufariki walisemekana kulalamika maumivu makali ya tumbo, pamoja na tumbo zao kujaa gesi.

Kulingana na taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti moja la taifa hilo la Afrika mashariki Jumatano, vifo hivyo vilitokea ndani ya wiki moja na kuzua maswali mengi kuliko majibu.

“Vifo vya watoto vimetokea kwa nyakati kuanzia Julai 5 hadi leo ambapo amefariki mtoto mwingine aliyekuwa mgonjwa baada ya kubaki pekee Hospitali ya Mkoa Arusha ya Mount Meru Arusha,” Diwani wa eneo hilo Nanga Mollel alinukuliwa.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa mtoto wa kwanza Bosi Nyangusi alifariki Julai 15, 2022 kutokana na kusumbuliwa na tumbo.

Mollel amesema baada wanzake wanne walipelekwa hospitali ya TMA Monduli na wakapata matibabu na kuruhusiwa ila wakiwa njiani walizidiwa na kupelekwa Mout Meru, ambapo Julai 16 alifariki Saimalie.

Amesema baadae watoto wawili walifariki Julai 17 ambao ni Lemali na Sophia.

Diwani huyo amesema Jumanne mtoto aliyekuwa amebaki amelazwa hospitali ya Mount Meru amefariki dunia ambaye ni Veronica aliyekuwa anasoma darasa la tatu Mswakini.

Baada ya vipimo, taarifa zilisema kwamba huenda kifo chao kilisababishwa kutokana na kula au kunywa kitu chenye sumu ila vyanzo vya ndani vilidai kwamba watoto hao walinyweshwa maziwa yenye sumu.

Makiwa kwa familia hiyo.