Mama na mwanawe wafariki baada ya kula viazi mwitu

Mhudumu wa afya alisema kwamba wagonjwa hao walikuwa wanaharisha na kutapika.

Muhtasari

• Mtoto mwingine wa mama huyo ambaye pia alivila viazi hivyo vilivyopikwa na mama bado yungali hospitalini baada ya kusalimika kifo.

Image: Screengrab YouTube

Mama mmoja ameripotiwa kufariki pamoja na mwanawe baada ya kula viazi vya mwituni ambavyo vilikuwa na sumu kali.

Katika taarifa iliyopakiwa kwenye mtandao wa YouTube, mwanamke huyo kwa jina Rehema Mkonomi na mwanawe Mariam Hassan ambao ni wakaazi wa kata ya Mlanzi Kibiti nchini Tanzania, walipatwa na umauti baada ya kushtaki njaa kwa viazi ambavyo mama huyo alivitoa porini.

Mtoto mwingine wa mama huyo ambaye pia alivila viazi hivyo vilivyopikwa na marehemu bado yungali hospitalini baada ya kusalimika kifo na anazidi kupigania maisha yake.

Wakaazi walieleza kwamba mama huyo alienda porini na kurudi na viazi hivyo ambavyo hakujua kuwa ni sumu na pindi alivyopika akapakua ili kula na wanawe.

“Alivyokula na watoto wake ndio akaanza kutapika pale, ndio wakachukua hatua ya kuenda hospitalini ambapo alipatiwa dawa na kurudi lakini ile dawa haikusaidia. Wakaanza kulewa na ndio tukachukua hatua ya kuwaleta hapa hospitali kuu,” bibi mmoja alieleza.

Mhudumu wa afya alisema kwamba wagonjwa hao walikuwa wanaharisha, kutapika na pia kuishiwa nguvu jambo ambalo lilipelekewa kutopeta nguvu nyingi mwili ni na kuitoa pumzi ya mwisho.

Wakaazi wengine wanahisi ni tabu ya njaa iliyosababisha wanafamilia hao kuvamia chakula hicho chenye sumu pasi na kujua kwani pia iliarifiwa walikuwa ni wageni katika eneo hilo.