Mwanamke ahukumiwa kifo kwa kumuua mama mjamzito na kutoa mtoto tumboni

Mwanamke huyo alikuwa hana kizazi na alikuwa amewadanganya jamaa zake kuwa ana ujauzito.

Muhtasari

• Muda mfupi kabla ya matukio, alikuwa ametazama video nyingi za kujifungua na sehemu za upasuaji.

• Alipokamatwa, alipatikana na mtoto huyo mchanga aliyesema ni wake amemzaa. Mtoto aliokolewa ila akafariki muda mchache baadae.

Kamba ya kujiua
Kamba ya kujiua
Image: Image: Courtesy

Mwanamke mmoja nchini Marekani amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mwanamke mwenzake aliyekuwa mjamzito na kutoa mtoto tumboni mwake.

Kulingana na jarida la AFP, mwakamke huyo kwa jina Taylor Parker mwenye umri wa miaka 29 alisemekana kuwa alichukua uamuzi wa kumuua mwakamke mjamzito na kutoa mtoto tumboni baada ya muda mrefu wa kumdanganya mpenzi wake wa kiume pamoja na marafiki kwamba alikuwa na ujauzito.

“Kwa muda wa miezi kadhaa Parker alimwambia mpenzi wake na jamaa zake kwamba alikuwa mjamzito. Alichapisha kuhusu hilo kwenye mitandao ya kijamii na kununua tumbo bandia la silicone. Yote yalikuwa ni uwongo. Ukweli ni kwamba alikuwa ametoa kizazi na hakuweza kupata mtoto,” jarida hilo liliripoti.

Kutokana na hali yake na kutokuwa na kizazi cha kumwezesha kubeba ujauzito, na ikizingatiwa kwamba alikuwa amewahadaa watu wa karibu kuwa ni mjamzito, alichukua uamuzi wa kutafuta njia mbadala ya kupata mtoto mchanga kwa njiayoyote ile – nalo jibu likamjia ni kumuua mwanamke na kutoa mtoto tumboni!

“Mnamo Oktoba 9, 2020, Parker alienda nyumbani kwa Reagan Simmons-Hancock, mjamzito mwenye umri wa miaka 21 katika miezi ya mwisho ya ujauzito wake, na kumchoma kisu zaidi ya mara 100. Baada ya kulikata tumbo lake ili kuchukua kijusi chake, aliondoka, akimuacha bintiye mwenye umri wa miaka 3 akiwa amelala katika chumba kingine. Parker alikamatwa muda mfupi baadaye akiwa kwenye gurudumu la gari lake takriban kilomita 15 kutoka kwa mauaji hayo. Mtoto mchanga alikuwa kwenye mapaja yake. Aliambia mamlaka kwamba alikuwa amejifungua tu. Mtoto alilazwa hospitalini lakini hakusalimika,” taarifa ilieleza.

Wiki chache kabla ya mauaji hayo, Parker alikuwa ameanza kuwatafuta wanawake wajawazito katika maduka na wodi za wajawazito, kulingana na ushahidi wa polisi kwenye kesi hiyo.

Muda mfupi kabla ya matukio, alikuwa ametazama video nyingi za kujifungua na sehemu za upasuaji.