Muhoozi atoa 'msamaha' hadharani kwa Yesu Kristo, "Nimekuwa na hasira hivi karibuni"

Muhoozi katika siku za hivi karibuni amekuwa akirumbana na watu kufuatia matamshi yake chochezi.

Muhtasari

• Mwezi Oktoba alichokoza Kenya akisema alikuwa na mpango wa kuiteka nyara Nairobi na kuishi sehemu ya Westlands.

KWA HISANI
KWA HISANI
Image: Muhoozi Kainerugaba

Mwanawe rais wa Uganda, Muhoozi Kainerugaba ametoa msamaha wa kibinafsi kwa Yesu Kristo kwa kile ambacho alisema ni kuwa na hasira katika siku za hivi karibuni.

Muhoozi Kainerugaba ambaye ni mkuu wa majeshi ya ardhini ya Uganda kupitia ukurasa wake wa Twitter, alisema hataki kumaliza mwaka akiwa na kinyongo na Mwana wa Mungu na kumtaka radhi kwa yote hasi ambayo amekuwa akizungumza na kufanya.

Baada ya mwaka wa matukio ambapo aliwachambua watu kadhaa kwa njia isiyo sahihi, Muhoozi amekiri hadharani kuwa amekuwa na masuala ya hasira.

“Ninataka kuwaomba wote msamaha. Yesu Kristo, Mungu wetu, ni mfanya amani. Ninamwomba msamaha kwa hasira yangu hivi karibuni,” Kainerugaba aliandika.

Katika tweets zake, Muhoozi alisema kwa asili yeye ni mtu wa amani, na kuongeza kuwa inahitaji uchokozi mwingi ili kumchafua.

Katika tweet zake za hivi majuzi zenye utata, Muhoozi alidai kuwa kama angekuwa Vladimir Putin, Rais wa Urusi, angeiteka Kyiv ndani ya wiki mbili, akiitaja kama kituo kidogo cha biashara.

Hata hivyo, saa chache baadaye Muhoozi alinyenyekezwa, ikiwa tweets zake zilikuwa za kupita.

Mapema Oktoba Muhoozi alitishia kuteka Nairobi kisha akauliza kwa kejeli mawazo ya wapi Nairobi anapaswa kufanya makazi yake baada ya kumaliza utekaji.

Katika tweet nyingine, alidai kuwa ‘kakake mkubwa’ aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta alimkatisha tamaa kwa kutowania muhula wa tatu afisini.

Pia alipendekeza kuwa mkuu huyo wa nchi mstaafu alipaswa kuazima jani kutoka kwa babake Rais Museveni ambaye amefaidika mara mbili na mabadiliko ya katiba.