Rais wa Uchina Xi Jinping ateuliwa kwa muhula wa tatu kama Rais

Jinping ni kiongozi mkuu wa nchi ya Kikomunisti ya Uchina.

Muhtasari

•Xi aliteuliwa Ijumaa kama rais tena kwa miaka mingine mitano na muhuri ya bunge la Uchina katika ukumbi mkuu wa watu wa Beijing.

Rais wa Uchina ,Xi Jinping, ameidhinishwa kwa muhula wa tatu kama Rais.Muhula wake uliidhinishwa na wasomi wa kisiasa wa nchi hiyo siku ya Ijumaa na kuimarisha udhibiti wake na kumfanya kuwa kiongozi wa nchi hiyo ya Kikomunisti aliyekaa muda mrefu tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 1949.

Xi aliteuliwa Ijumaa kama rais tena kwa miaka mingine mitano na muhuri ya bunge la Uchina katika ukumbi mkuu wa watu wa Beijing.Alipata kura 1,952 kwa kauli moja na kufwatiwa na shangwe.

Nguvu ya Xi inatokana na yeye kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti na Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Kijeshi (CMC). Kuthibitishwa kwa muhula wake wa tatu kama rais kulitarajiwa na wengi.

Kutajwa kwa waziri mkuu mpya na mawaziri mbalimbali katika siku zijazo kunachukuliwa kuwa muhimu zaidi. Wateule wapya wote wanatarajiwa kuwa watiifu wa Xi Jinping. Hii ni pamoja na Li Qiang, ambaye anapendekezwa kuhudumu kama nambari ya pili ya Rais Xi.

 Jinping ameimarisha utawala wake wakati Uchina inafungua tena kutoka kwa sera yake ya sifuri ya Covid ambayo imechochea maandamano dhidi ya serikali. Kinachojulikana kama Vikao Viwili vya Bunge la Kitaifa la Umma na Baraza la Ushauri la Kisiasa la Watu wa China (CPPCC) wiki hii vinafuatiliwa kwa karibu huku vikitoa taswira ya mwelekeo wa China katika miaka ijayo.

Tangu Mao Zedong, viongozi nchini China walikuwa wamewekewa mihula miwili tu madarakani. Bw Xi alipobadilisha kizuizi hiki mnamo 2018, kilimbadilisha kuwa mtu ambaye hajawahi kuonekana tangu Mwenyekiti Mao.