Papa Francis asema viongozi wa makanisa ya Afrika wanaona mapenzi ya jinsia kwa mtazamo wa kitamaduni kama "kitu kibaya"

Kulingana na Papa maaskofu wa Afrika ni 'kesi maalum' kuhusu baraka za wapenzi wa jinsia moja.

Muhtasari

• Papa Francis amesema maaskofu wa Kiafrika ni "kesi maalum" kuhusiana na upinzani wao kwa uamuzi wake wa kuruhusu baraka kwa wapenzi wa jinsia moja.

Papa Francis
Image: BBC

Papa Francis amesema maaskofu wa Kiafrika ni "kesi maalum" kuhusiana na upinzani wao kwa uamuzi wake wa kuruhusu baraka kwa wapenzi wa jinsia moja.

Lakini alibaki na uhakika kwamba hatua kwa hatua kila mtu atahakikishiwa na tamko la Kanisa.

Katika mahojiano na gazeti la Italia, Papa alisema viongozi wa makanisa ya Afrika na wafuasi wao wanaona mapenzi ya jinsia moja kutoka kwa mtazamo wa kitamaduni kama "kitu kibaya".

Alisema hati mpya ya mwezi uliopita, Fiducia Supplicans, ilikusudiwa "kuunganisha na sio kugawanya".

Papa Francis alisema hajali kuhusu wahafidhina kujitenga na Kanisa Katoliki kutokana na mageuzi yake, akisema kuwa mazungumzo ya mgawanyiko yanaongozwa na kile alichokiita "makundi madogo ya itikadi".