Waziri mkuu wa Congo amejiuzulu siku 8 baada ya kuthibithishwa kwa mamlaka yake

Waziri Mkuu aliwasilisha kujiuzulu kwake kwa Rais Felix Tshisekedi siku nane baada ya kuthibitishwa kwa mamlaka yake kama naibu wa kitaifa.

Muhtasari

• Lukonde aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo ya Afrika ya kati yenye utajiri wa madini mnamo Februari 2021.

Jean-Michel Sama Lukonde
Jean-Michel Sama Lukonde
Image: x

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jean-Michel Sama Lukonde, alijiuzulu siku ya Jumanne, na kusababisha kuvunjwa kwa serikali yake, ofisi ya rais ilisema katika taarifa yake kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Waziri Mkuu aliwasilisha kujiuzulu kwake kwa Rais Felix Tshisekedi siku nane baada ya kuthibitishwa kwa mamlaka yake kama naibu wa kitaifa.

Sasa atajiunga na bunge kama mjumbe wa bunge hilo.

"Kujiuzulu kumekubaliwa. Hata hivyo, rais ameiomba serikali (ya Lukonde) kuendelea kushughulikia masuala ya sasa" hadi serikali mpya itakapoundwa, ofisi ya rais ilisema katika taarifa nyingine baadaye Jumanne, Reuters waliripoti.

Haikueleza sababu za Lukonde kujiuzulu.

Lukonde aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo ya Afrika ya kati yenye utajiri wa madini mnamo Februari 2021.

Baada ya kuchaguliwa tena Desemba, Tshisekedi alimteua mwakilishi wa kubainisha muungano wa wengi ndani ya Bunge la Kitaifa kwa nia ya kuunda serikali ijayo.