Mwanaume afariki baada ya kijichoma moto nje ya mahakama iliyokuwa ikiendesha kesi ya Trump

Maxwell Azzarello, 37, alijimwagia mafuta kabla ya kurusha hewani vijikaratasi vya nadharia ya njama.

Muhtasari

•Tukio hilo lilitokea wakati uteuzi wa mahakama kwa ajili ya kesi ya Bw Trump ulipokamilishwa.

Image: BBC

Mwanamume mmoja aliyejichoma moto nje ya mahakama ya Manhattan ambako kesi ya rais wa zamani Donald Trump inashikiliwa amefariki.

Maxwell Azzarello, 37, alijimwagia kimiminika kabla ya kurusha hewani vijikaratasi vya nadharia ya njama.

Tukio hilo lilitokea wakati uteuzi wa mahakama kwa ajili ya kesi ya Bw Trump ulipokamilishwa.

Alipelekwa hospitalini siku ya Ijumaa akiwa katika hali mbaya, ambapo baadaye alifariki, Habari za CBS - chombo cha habari washirika wa BBC wa Marekani - kilithibitisha.

Bw Trump alikuwa katika jumba hilo kuhudhuria uteuzi wa mahakama, ambapo amekuwa na taarifa za usalama, lakini rais huyo wa zamani aliondoka wakati wa kisa hicho.

Polisi wa jiji la New York walisema mapema Jumamosi kwamba wafanyakazi wa hospitali walitangaza kifo cha Bw Azzarello , NBC iliripoti.