Nyota wa 'Pirates of the Caribbean' auawa katika shambulio la papa

Lakini Perry, ambaye pia alikuwa afisa wa uokoaji maisha ufuoni , alitangazwa kuwa amekufa na wahudumu wa afya baada ya kuletwa ufukweni .

Muhtasari
  • Nyota huyo mwenye umri wa miaka 49 alifariki Jumapili mchana, huduma za dharura za Honolulu zilithibitisha katika mkutano na waandishi wa habari.

Mwigizaji wa Pirates of the Caribbean Tamayo Perry amefariki dunia baada ya kushambuliwa na papa alipokuwa akijivinjari kwenye mawimbi huko Hawaii.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 49 alifariki Jumapili mchana, huduma za dharura za Honolulu zilithibitisha katika mkutano na waandishi wa habari.

Huduma za dharura ziliitwa hadi Malaekahana Beach karibu 13:00 saa za ndani.

Lakini Perry, ambaye pia alikuwa afisa wa uokoaji maisha ufuoni , alitangazwa kuwa amekufa na wahudumu wa afya baada ya kuletwa ufukweni .

Perry aliigiza kama mmoja wa wababe katika filamu ya Pirates of the Caribbean: On Stranger Tides, filamu ya nne katika mfululizo huo.

Filamu hiyo ya 2011, ambayo inamhusu Johnny Depp kama maharamia Captain Jack Sparrow, pia ina nyota kama vile Penelope Cruz na Geoffrey Rush.

Perry piaaliigiza katika filamu za Lost, Hawaii Five-0, Blue Crush na Charlie's Angels 2, na alionekana katika tangazo la Coca-Cola.