Mtoto ni wa nani?

Nilikuwa na wapenzi kadhaa sasa sijui aliyenipa mimba –Mwanamke

Hawajui wanaompa mimba kwa sababu kila wakati ana zaidi ya mpenzi mmoja katika uhusiano .

Muhtasari
  • Tatizo ni kwamba hakujua mimba ile ilikuwa ya nani kati ya takriban wanaume watatu ambao alikuwa na mahusiano nao .
  •  Baadye wakati alipoona hatari ndipo alipoanza mwendo kujipeleka hospitalini .

 

Mwiba wa kujitakia  haumbiwi pole lakini mimba ya kujitakia utaishughulikia vipi?

 Ndio kizungumkuti kinachokumba maisha ya Jocelyn ambaye  amekoa uthibiti wa kimwili na  hadi  sasa ameavya mimba zaidi ya mara mbili –kisa na maana? Hawajui wanaompa mimba kwa sababu kila wakati ana zaidi ya mpenzi mmoja katika  uhusiano .

 Jocelyn sio pekee yake katika hali kama hii kwa sababu idadi ni kubwa ya wanawake wadogo ambao hamu zao za kimwili hazitoshelezwi katika uhusiano mmoja sasa mtindoi unakuwa wa fungua fungua ya hapa na pale na licha ya kutumia njia nyingi kuzuia mimba , aghalabu inatokea kwamba bao limefungwa wakati mlinda lango amezubaa .

 Jocelyn  anasema alipopata mimba ya kwanza alifahamu aliyempa mimba hiyo lakini hakuwa tayari kuwa mama na akaitoa kwa njia ya kijanja huku akiwadanganya wote waliojua kwamba ana mimba kwamba  ilitoka kwa bahati mbaya  baada yay eye kuanguka . Baadye hata hivyo inabainika kwamba aliavya mimba hiyo baada ya kuanza kutofautiana na mpenzi wake wa wakati huo . Hakuona mustakabli  mzuri na akilini mwake aliona kuitoa mimba ile ndio njia pekee na bora wakati huu kujiacha kuwa huru .

 Kando na hatari iliyokuwepo , Jocelyn hakutilia ,mwili wake ukikemaa tena na kujipata tena katika uhusiano zaidi ya mmoja na wanaume tofauti . Fungua fungua za hapa na pale zilitumbukia tena yeye kupata mimba ambayo hakuwa amepanga kuipata . Kwa sababu ya kwanza aliitoa bila  tatizo wala hofu ya kujibu  swali lolote ,basi ilikuwa sasa mazoea .Alifuata mtindo wa kwanza na kuiavya mimba ile kwa tembe ya kujininulia dukani .

Tatizo ni kwamba hakujua mimba ile ilikuwa ya nani kati ya takriban wanaume watatu ambao alikuwa na mahusiano nao . Ilizuka sakata ambapo jamaa zake wengi walimgeuka kwa sababu walitaraji kwamba alipata funzo kutokana na janga lilimpata mara ya kwanza na kisa cha pili akiavya mimba nusra angeaga dunia kwa sababu abaada ya kuvuja damu mchana wote na akuua kilichokuwa kikifanyika alinyamaza . Baadye wakati alipoona hatari ndipo alipoanza mwendo kujipeleka hospitalini .

  Jocelyn anasema hajui kinachomingia fikrani wakati anapopona na kupata nafuu kwani anajikuta tu katika mahusiano hayo ya kujihusisha na wanaume bila kujali kuhusu matokeo yake hadi wakati sakata kama hiyo inapomfikia .