Wanawake katika ulimwengu unaobadilika wa kazi; Kazi zilizoonekana kuwa tambiko enzi za kale zikifanywa na wanawake

Muhtasari
  • Kuna pengo kubwa la jinsia katika mapato na mishahara, hata baada ya kudhibiti sekta na kazi
  • Moja wapo ya sababu kuu zinazochangia pengo la mishahara katika kazi ya mishahara ni mgawanyo wa kikazi
Image: Hisani

Hakuna kizuizi, hakuna kizuizi, na hakuna mpaka wenye nguvu za kutosha kumzuia mwanamke kufikia kile anachotaka. Leo, kwa mwanamke, kizuizi pekee ni ndoto na matarajio yake.

Ikiwa wewe ni mwanamke, elewa kwamba hakuna kizuizi cha kutimiza ndoto zako. Lakini kwa sababu mbalimbali, unaweza kuwa na machafuko kuhusu ni kazi gani zinazoweza kuwa bora kwa wanawake.

Ingawa inatofautiana kulingana na mahitaji maalum ya kila mwanamke, kazi bora za wanawake zinaweza kupunguzwa.

Kuna pengo kubwa la jinsia katika mapato na mishahara, hata baada ya kudhibiti sekta na kazi.

Wanawake kwa wastani hupata kati ya asilimia 10 na asilimia 30 chini ya wanaume wanaofanya kazi lakini kuna tofauti kubwa kati ya nchi

Moja wapo ya sababu kuu zinazochangia pengo la mishahara katika kazi ya mishahara ni mgawanyo wa kikazi.

Wanawake na wanaume hupata mishahara tofauti kimsingi kwa sababu ya aina tofauti za kazi wanazofanya.

Takriban nchi zote, wanawake wana uwezekano mkubwa wa kushiriki katika shughuli za uzalishaji mdogo kuliko wanaume. Pia wana uwezekano mkubwa wa kuwa katika ajira ya ujira au isiyolipwa ya familia au kufanya kazi katika sekta isiyo rasmi ya ujira.

Katika ajira rasmi, wanajikita katika kazi na sekta za "kike". Mitindo hii ya ubaguzi wa kijinsia katika shughuli za kiuchumi inabadilika na maendeleo ya kiuchumi lakini haipotei.

Historia ya kazi na mishahara ya wanawake na jinsi imeleta mafanikio kwa ajili yetu sote;

 Kuwapa wanawake haki ya kupiga kura, tunapaswa pia kusherehekea hatua kubwa ambazo wanawake wamepiga katika soko la ajira.

Kuingia kwao katika kazi ya kulipwa kumekuwa sababu ya kutimiza mahitaji yao na kujikimu kimaisha.

Wanawake wamezoewa kufanya kazi kama Wasaidizi wa matibabu.kufundisha,kijakazi,ususi nk.

Katika enzi za akina babu zetu kuna baadhi ya kazi ambazo wanawake hawangefanya kwani zilikuwa tambiko kwa jamii.

Katika karne hii ya sasa kuna baadhi ya wanawake ambao wamejikakamua na kutupilia mbali tambiko hizo ili kujikimu maishani na kuweka mkate wa kila siku kwa familia zao.

Kwa hakika wanawake wengi wamekaza kamba na ufanya kazi hizi licha ya changamoto nyingi wanazopitia kama wanawake.

Ndio kazi hizo zilikuwa zinafanywa na wanaume, katika makala haya tutaangazia kazi hizo, na changamoto ambazo wanawake hao wanapitia.

Baadhi ya kazi hizo ni pamoja na;

1.Kushona na kusafisha viatu

Ni kazi ambayo ilitambuliwa kuwa ya wanaume na wala sio wanawake, unapotembea jijini Nairobi utawaona wanawake wengi wakisafisha viatu vya wateja.

Nikiwa kwenye ziara yangu nilipatana na Monica ambaye ni mshona viatu na alikuwa na haya ya kusema.

"Kazi yangu niliianza miaka 2 iliyopita, na ndio inanilipia nyumba na kunikimu, hii ni baada ya kusimamishwa kazi, na kwa maana nilikuwa na ujuzi wa kushona viatu nilianza kushona

Ndio kuna changamoto kadhaa kama vile mteja kukuletea kiatu unashona kisha anapotea kabisa, ilhali umetumia bidahaa zako

Hii ni kazi ambayo inadharauriwa sana, lakini mimi naitambua sana, na wala huna shinikizo na nikazi ambayo inakupa wakati wa kufanya mambo mengine."

2.Kondakta

Wengi wakiwaona wanawake kwenye sekta hii hushtuka sana, kwani ata wakati wa enzi za akina babu zetu wanaume ndio walitambuliwa sana kwa kazi hii.

Gillian, ni Kondakta abaye anatambua na kuthamini kazi yake;

"Baada ya mume wangu kuaga dunia sikuwa na namna nyingine, ila kutafuta kazi ambayo itanikimu pamoja na na watoto wangu, hii ni kanairo na ukilalisha macho utakuwa omba omba kila wakati

Ni kazi ambayo ina changamoto zake, kama kwa mfano mwanamume anakuona na anakudharau kisha anazusha akilipa nauli kwa sababu wewe ni mwanamke

Pia changamoto nyingine ni wakati wa kufungua azi asubuhi mapema, na watoto bado wanakutegemea na pia wakati wa kufunga kazi kama saa tano ndio unafika kwa nyumba na una watoto

Lakini yote namshukuru Mungu kwa sababu kama sio yeye huwezi kuwa mshindi kwenye changamoto hizi.

3.Dereva wa Texi

Asilimia kubwa ya wanawake wamesalia nyumbani huku waume wao wakitafuta riziki kupitia kazi hii ya texi. lakini baadhi yao wwameamua kuwa hawatalala njaa ila kuanza kufanya kazi hii.

Licha ya kuwa na changamoto nyingi, wanawake kadha wa kadha wamejitahidi na kuanza kazi hii.

Huku nikizugumza na Carol,alisema kwwamba ni kazi ambayo ina starehe zake licha ya kukumbana na changamoto.

"Kwanza changamoto ya kwanza ni kuwa unapoenda kuoshewa gari utapatana na madereva wanaume ambao wanakudharau na kuona kwamba hujui kuendesha vyema na kukupita, ila wakati huo unahitaji kuoshewa gari ili ukabebe mteja wako

Changamoto ya pili ni ukiwa umebeba mteja kuna baadhi ya wanaume watajaribu kukushika kwa mapaja, wengine pia watakataa kukulipa licha ya kuitisha texi na kuchoma mafuta yako

Lakini ukijua kufanya kazi hii utafurahia matunda yake."

4.Kuendesha pikipiki

Tekla alisema kuwa;

"KUpata wateja utapata lakini unaweza kuwa umejieka kwa mtego kwa maana sio kila mtu ambaye ana nia njema kukuhusu. ni kazi ambayo haikutambuliwa sana kwa maana akina babu zetu waliamini kwamba kazi ya mwanamke ni kukaa nyumbani na kuwatunza watoto wake na mumewe

Kwa kweli nilipoanza kazi hii nilipata changamoto za hapa na pale lakini nimeifanya kwa miaka 5 sasa, lakini cha muhimu ni kuwa napataa pesa

Pia nilipoanza kazi hii mengi yalisemwa lakini singeweza kutegemea pesa za mtu mmoja,uzuri wa waendesha pikipiki wana umoja, ambao ulinifurahisha, si kutafuta tu kazi bali nilitafuta kazi ambayo ina umoja na amani."

Kwa hivyo tukimalizia makala haya tunaweza kusema kwamba hamna kazi ambayo mwanamke hawezi kufanya licha ya kazi nyiingi kutamkwa na kuaminika kuwa za wanaume.

Haya basi hawakukosea waliposema kazi ni kazi ata kama ni chomela, bora hujikimu maishani.

Je maoni yako ni yapi kuhusu wanawake kufanya kazi ambazo ziliaminika kuwa tambiko enzi za kale?