Fahamu sababu zinazochangia baadhi ya watu kukosa furaha

Muhtasari

•Kwa miongo kadhaa watafiti walifanya tafiti wakitumia mapacha na kubaini kuwa ni jeni zinaeleza jinsi furaha ya inatofautiana kwa asilimia 40 hadi 50

Image: getty images

Sekta za kujitegemea zinazidi kushamiri. Zimekuwa zikipata kasi kwa miaka kutoknaa na kuwa na saikolojia chanya, utafiti wa kisayansi kuhusu kile huchangia watu kuendelea. Wakati huo huo viwango vya wasi wasi, huzuni na kujidhuru vinaongezeka duniani. Tmehukumiwa tusiwe na furaha licha ya hatua hizi za kisaikolojia?

Tunapozungumza kuhusu saikolojia chanya, tukumbuke makala yaliyochapishwa kwenye jarida la Mapitio ya Saikolojia ya Jumla mwaka 2005, yaliyobadilisha jinsi tulikuwa tunaona furaha yetu.

Utafiti huo ulifichua kuwa asilliamia 50 ya furaha ya watu hutokana na jeni zao, asilimia 10 hutegemea hali zao na asilimia 40 hutegemea shughuli wanazofanya.

Kwa miongo kadhaa watafiti walifanya tafiti wakitumia mapacha na kubaini kuwa ni jeni zinaeleza jinsi furaha ya inatofautiana kwa asilimia 40 hadi 50

Hii ni mbinu ya kungalia jenetiki na mazingira ya watu katika misingi ya mahusiano ya kifamilia ndio sababu mapacha wanatumiwa hapa.

Tatizo ni kwamba, walidhani kuwa mapacha wa kufanana na mapacha uhisi mazingira sawa wanapokulia pamoja, suala ambalo halina ukweli.

Ili kujibu ukosoaji ya makala hiyo ya mwaka 2005, waandishi wale wale waliandika makala nyingine mwaka 2019 iliyoeleza kwa njia tofauti athari za jeni kwa furaha yetu, ikitambua mwingiliano kati ya jeni zetu na mazingira yetu.

Asili na elimu

Asili na malezi havitegemeani.

Jeni hushawishi tabia inayosaidia watu kuchagua mazingira yao. Kwa mfano jeni zilizopitishwa kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto husaidia watoto kujenga vikundi vya marafiki.

Image: GETTY IMAGES

Vile vile mazingira hubadilisha tabia za jeni.

Kwa mfano, akina mama wanaokumbwa na hasira wakati wakiwa wajawazito, jeni za watoto wao hubadilishwa na kuchangia mabadiliko ya kemikali inayoathiri ukuaji wa mtoto.

Kutokana na hilo watoto huzaliwa wakiwa wadogo wakikiwa na matatizo kama vile ugonjwa wa moyo.

Hii ndio sababu ya watu wawili wanaolelewa mazingira sawa wanaweza kujibu kichocheo sawa kwa njia tofauti.

Wengine huchangia mazingira yao kwa hivyo wanaweza kubadilisha sana mawazo yao, hisia na tabia kuambatana na hali mbaya au nzuri.

Kwa hivyo wakati wanahudhuria semina za ustawi au wanaposoma kitabu kinachohusu saikolojia nzuri, wanaweza kuchochewa na kubadilika wakilinganishwa na wengine. Pia mabadiliko hayo yanaweza kudumu kwa muda mrefu.

Image: GETTY IMAGES

Lakini hakuna saikolojia nzuri inayofanya kazi kwa kila mtu kwa sababu tuna tofauti ya DNA. Hivyo ni kusema tuna viwango tofauti vya ustawi na mabadiliko yake katika maisha.

Pia iwapo watu wanaweza kuwa na furaha hutegemea mazingira yao. Hii ni kulinga na uwezo wao wa kubadilika.

Tunaelekea mkondo wa kukosa furaha

Baadhi ya watu lazima wapambane zaidi kuboresha ustawi wao kuliko wengine na mapambano hayo yanamaanisha kuwa hawana furaha kwa kipindi kirefu.

Katika viwango vya chini sana, hawawezi kamwe kushuhudia furaha ya hali ya juu.

Tofauti ni kwamba wale walio na uwezo wa kubadilika kuambatana na mazingira yao wanaweza kuboresha ustawi wao na hata kupiga hatua zaidi ikiwa watachagua mtindo wa maisha wenye afya na kuishi katika mazingira yanayochochea furaha zao.

Kilicho muhimu pia ni maamuzi tunayofanya kuhusu maeneo tunamoishi, kina nani tunaishi nao na vile tunaishi maisha yetu, vyote vinaathiri furaha zetu na furaha za vizazi vyetu vinavyokuja.