Opinion:Je Serikali inafanya juhudi za kutosha kukabliana na uhaba wa mafuta nchini

Muhtasari
  • Je Serikali inafanya juhudi za kutosha kukabliana na uhaba wa mafuta nchini
Image: Ezekiel Aming'a

Hata baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutia saini makadirio ya ziada ya bajeti ya 2021-2022 kuwa sheria inayosafisha njia ya kutolewa kwa Ksh.34 bilioni kwa kampuni za uuzaji wa mafuta (OMCs), wananchi wanakabiliana na uhaba wa mafuta.

Kuidhinishwa kwa mswada huo kunaonekana kuwa wakati mwafaka katika kutatua uhaba wa mafuta uliopo ambao umehusishwa na uhifadhi wa bidhaa na OMCs huku wakishinikiza malipo ya malimbikizo kutoka kwa ruzuku ya mafuta.

Mgogoro huo wa malipo umesababisha uhaba mkubwa wa mafuta kote nchini huku madereva na waendesha bodaboda wakipanga foleni kwa saa nyingi ili kupata bidhaa hiyo muhimu.

NI takriban zaidi ya siku 4 sasa tangu madereva wa tex na waendesha moda moda kulalamikia uaba wa mafuta nchini, huku foleni ndefu kwenye vituo vya mafuta vikishuhudiwa.

Siku ya Jumanne madereva walionekana kwenye vituo vya mafuta wakifunga foleni ndefu, huku baadhi yao wakisema kwamba wamekosa mafuta kwa siku tatu ata licha ya kufunga foleni, huku wakiwa na matumaini ya kupata mafuta na kuendelea na biashara zao.

Baadhi yao wanasema kwamba wameamka usiku wa manane ili kupata mafuta bali hawajaweza kufanikiwa.

Mgao kutoka kwa bajeti ya ziada unatarajiwa kufidia malipo ya Ksh.13 bilioni zinazodaiwa na wauzaji soko kulingana na Wizara ya Petroli huku salio likitarajiwa kulipa malipo yajayo kutoka kwa ruzuku.

Kutiwa saini kwa makadirio ya bajeti kunatarajiwa sasa kufungua njia ya kumaliza tatizo la uhaba wa mafuta kwa kuruhusu kutolewa kutoka hazina hadi ruzuku.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii wafanyakazi wa vituo vya mafuta, walionekana kusherehekea siku ya Jumatatu usiku baada ya lori kuwasili likiwa limebeba mafuta.

Uhaba wa mafuta umeathiri kila mwananchi kwa njia tofauti.

Je unadhani kuwa serikali inafanya juhudi kukabiliana na uhaba wa mafuta nchini?