Orodha ya viongozi wa kigeni waliohudhuria misa ya hayati Mwai Kibaki katika Nyayo Stadium

Muhtasari

•Misa hiyo ilianza mwendo wa saa tano na inatarajiwa kuisha wakati wowote kuanzia saa nane alasiri.

•Zaidi ya viongozi 8 wa mataifa ya kigeni ni miongoni mwa wageni waliohudhuria ibada ya kumpungia Kibaki mkono wa buriani.

Misa ya Hayati Mwai Kibaki yaendelea katika uwanja wa Nyayo mnamo Aprili 29,2022
Misa ya Hayati Mwai Kibaki yaendelea katika uwanja wa Nyayo mnamo Aprili 29,2022
Image: EZEKIEL AMINGA

Misa ya mazishi ya rais wa tatu wa Kenya hayati Emillio Mwai Kibaki inaendelea katika uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi.

Misa hiyo ilianza mwendo wa saa tano na inatarajiwa kuisha wakati wowote kuanzia saa nane alasiri.

Ibada hiyo ya kitaifa  imehudhuriwa na watu kutoka matabaka mbalimbali na vilevile nchi tofauti.

Rais Kenyatta aliwasili ugani Nyayo mwendo wa saa nne unusu asubuhi na kupokelewa na naibu wake William Ruto.

Zaidi ya viongozi wanane wa mataifa ya kigeni ni miongoni mwa wageni waliohudhuria ibada ya kumpungia Kibaki mkono wa buriani.

Orodha:-

1. Cyril Ramaphosa- Rais wa Afrika Kusini

2. Salva Kirr- Rais wa Sudan Kusini

3. Sahle-Work  Zewde- Rais wa Ethiopia.

4. Edward Ngirete- Waziri Mkuu wa Rwanda

5.  Philip Mpango- Naibu Rais wa Tanzania

6. Constantino Chiwenga- Naibu Rais wa Zibambwe

7. Jesicca Alupo- Naibu Rais wa Uganda

8. Joyce Banda- Aliyekuwa Rais wa Malawi

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa,Rais wa Ethiopia Sahle-Work Zewde,Rais wa Sudan Kusini Salva Kir na Rais Uhuru Kenyatta wakiwa katika uwanja wa Nyayo wakati wa mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Rais Mwai Kibaki Aprili 29,2022
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa,Rais wa Ethiopia Sahle-Work Zewde,Rais wa Sudan Kusini Salva Kir na Rais Uhuru Kenyatta wakiwa katika uwanja wa Nyayo wakati wa mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Rais Mwai Kibaki Aprili 29,2022
Image: ENOS TECHE

Rais Uhuru Kenyatta alitangaza habari za kifo cha aliyekuwa mtangulizui wake, Mwai Kibaki Ijumaa ya wiki jana.

Siku tatu, Jumatatu, Jumanne na Jumatano zilitengwa kwa umma kuona mwili wa hayati na kumpatia heshima za mwisho.

Hayati atazikwa Jumamosi nyumbani kwake katika eneo la Othaya, kaunti ya Nyeri.