Wanasayansi wataka kufahamu iwapo mimea inaweza kupandwa mwezini

Wanaanga wa NASA wanajaribu kupanda mimea mwezini, katika mpango mpya ambao umeanza kutekelezwa.

Muhtasari

•Ujumbe wa NASA wa Artemis 3 kwenda mwezini umeweka lengo la 2026 la utekelezaji wa mpango huu.

Image: BBC

Wanaanga wa NASA wanajaribu kupanda mimea mwezini, katika mpango mpya ambao umeanza kutekelezwa.

Ujumbe wa NASA wa Artemis 3 kwenda mwezini umeweka lengo la 2026 la utekelezaji wa mpango huu. Kwa sasa, wanasayansi wanataka kuelewa jinsi mwezi unaundwa na mabadiliko yanayotokea ndani yake, kutathmini ikiwa mwanadamu anaweza kuishi mwezini.

Sasa, NASA imetangaza kuwa itafanya tafiti tatu wakati wanaanga hao watakafanya safari yao ijayo ya mwezini.

Sehemu ya utafiti huu imedhamiria kuchunguza jinsi mwezi unavyosonga, ikiwa kuna matetemeko ya ardhi, ikiwa maji au barafu inaweza kupatikana kwenye ardhi ya mwezi na pia cha muhimu zaidi ni kwamba kuna mimea juu ya mwezi, na inaweza pia kukua vizuri.

Je, ujumbe wa Artemis kwenda mwezini unahusu nini?

Ujumbe huo unaoitwa Artemis kwenda mwezini una hadi miradi mitatu, ambayo ilipangwa na shirika la safari za anga za juu la Marekani NASA.

Madhumuni ya operesheni hii ni kuleta data zaidi kutoka mwezini kwa matumaini kwamba operesheni hiyo itafanyika mnamo 2026, wakati miaka 50 itakamilika tangu mara ya kwanza wanadamu kutua kwenye ardhi ya mwezi.

Ikiwa misheni hiyo itafaulu, wanasayansi hao wanatumai kwamba chombo hicho kitaweza kujenga makao ya kudumu ya binadamu kwenye ardhi ya mwezi.

Sehemu ya kwanza ya misheni hii ilifanyika mnamo 2022, wakati huo wanasayansi na wahandisi wanaofanya kazi kwenye mradi huu walikuwa wakihakikisha kuwa vifaa na vitu ambavyo vitatumika katika misheni ya Artemi ya baadaye vinafanya kazi ipasavyo.

Katika mwaka wa 2025, NASA itatuma roketi angani ili kuthibitisha sehemu ya pili ya misheni hiyo, ambayo inatarajiwa kuruka kuzunguka mwezi na kisha kurudi kwenye sayari ya Dunia.

Awamu ya mwisho ya misheni hii, inayoitwa Artemis 3, inatarajiwa kufanyika mwaka wa 2026, na itaendelea kama ilivyopangwa kwa hadi siku 30.

Utafiti wa Artemis 3 ni nini?

Wakati wa misheni ya Artemis 3, wanaanga waliochaguliwa kuwa sehemu ya misheni hiyo watakuwa na kazi ya kuchunguza mambo matatu.

Wataanzisha kituo cha ufuatiliaji wa mazingira ya mwezi, kubeba seismometer. Chombo hicho kinatumiwa na wanasayansi kupima matetemeko ya ardhi kwenye mwezi, na pia itakusanya habari nyingi kuhusu mwezi na zaidi.

Pia watajua ikiwa kuna uwezekano kwamba ardhi ya mwezi unaweza kupandwa mimea. Pia wataangalia nguvu za mwezi na anga yake.

Kwa kutumia chombo hicho, watachunguza mwezi kwa ajili ya maji na barafu, ambayo ikipatikana inaweza kuwa chanzo cha maji ya kunywa au mafuta ya satelaiti.