Yote unayopaswa kujua kuhusu Eid ul-Fitr na kwa nini tarehe ya kuadhimishwa hubadilika

Kuanza kwa Eid ul-Fitr kunafuatia mwisho wa Ramadhani, mwezi mtukufu wa mfungo unaofanywa na Waislamu kuanzia macheo hadi machweo kila siku.

Muhtasari

• Tarehe ya Eid al-Fitr inabadilika kutokana na tofauti kati ya kalenda ya jua ya Gregorian na kalenda ya Hajri, ambayo hutawaliwa na muda ambao mwezi huchukua kupitia kila awamu yake ya mwezi.

• Hii ina maana kwamba tarehe ya Eid ul-Fitr haijawekwa katika kalenda ya Gregorian.

• Katika siku ya Eid, Waislamu hutoa sadaka maalum kwa jina Zakat ul-Fitr.

Wasomi wa Kiislamu wamesema kuwa mwisho wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan unapaswa kutangazwa na KadhiImage
Wasomi wa Kiislamu wamesema kuwa mwisho wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan unapaswa kutangazwa na KadhiImage
Image: BBC

Aprili 10, 2024 imetangazwa kuwa sikukuu nchini Kenya kuwaruhusu waumini wa dini ya Kiislamu kuadhimisha siku ya Eid ul-Fitr.

Lakini je, sherehe za Eid ul-Fitr ni nini na kwa nini tarehe ya kuadhimishwa mwaka huu si sawa na tarehe ya mwaka jana, na mbona tarehe hizo hubadilika kila mwaka?

Pata majibu yote katika malaka hii.

Kwa mujibu wa mwandishi wa vitabu vya Kiislamu,  siku ya Eid ni sikukuu inayofanywa na Waislamu kusherehekea mwisho wa Ramadhani, mwezi mtukufu wa Kiislamu, ambapo Waislamu hufunga kila siku kati ya mawio na machweo.

Inayojulikana kama Eid ul-Fitr, ambayo ina maana ya 'Kuvunja Mfungo', inaangukia siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal katika kalenda ya Kiislamu.

Kuanza kwa Eid ul-Fitr kunafuatia mwisho wa Ramadhani, mwezi mtukufu wa mfungo unaofanywa na Waislamu kuanzia macheo hadi machweo kila siku.

Ramadhani, mwezi wa mwandamo, ni siku 29 au 30. Ilianza jioni ya Jumapili Machi 10 mnamo 2024, ambayo inamaanisha kuwa itaisha Jumatatu Aprili 8 2024, siku ya 29, au siku ya 30, Jumanne Aprili 9 2024.

Baada ya maombi ya machweo ya jua Jumatatu Aprili 8, ambayo ni siku ya 29 ya Ramadhani kwenye kalenda ya Shawwal, watazamaji wa mwezi wataelekea magharibi ili kujaribu kupata mtazamo wa kwanza wa mwezi mpevu.

Ikiwa mwezi mpya unaonekana, basi siku inayofuata itakuwa Eid, ikiwa sio, basi Waislamu watafunga siku moja zaidi kukamilisha mwezi wa siku 30.

Siku za kuadhimisha Eid hutofautiana kutoa taifa moja hadi lingine kutegemea na muonekano wa mwezi kutoka magharibi, tangazo ambalo aghalabu hutolea na imamu mkuu wa Kiislamu.

Tarehe ya Eid al-Fitr inabadilika kutokana na tofauti kati ya kalenda ya jua ya Gregorian na kalenda ya Hajri, ambayo hutawaliwa na muda ambao mwezi huchukua kupitia kila awamu yake ya mwezi.

Hii ina maana kwamba tarehe ya Eid ul-Fitr haijawekwa katika kalenda ya Gregorian.

Katika siku ya Eid, Waislamu hutoa sadaka maalum kwa jina Zakat ul-Fitr.

Zakat ul-Fitr, au Zaka ya Kufungua Mfungo wa Ramadhani, ni sadaka maalum ya faradhi inayotolewa na Waislamu wote mwishoni mwa mfungo wa mwezi wa Ramadhani, anaeleza mwandishi mwingine, Zac Campbell kwenye Daily Mail.

Pia inaitwa Sadaqat al-Fitr "Sadaka ya Kufungua Saumu" ya Ramadhani na Waislamu wanapaswa kutoa sehemu ya mali zao kwa wale wanaohitaji.

Ikiwa unataka kumtakia mtu unayemfahamu Eid njema, unaweza kusema: 'Eid mubarak' kwao.

Inapotafsiriwa kwa Kiswahili, inamaanisha 'sherehe iliyobarikiwa' au 'sikukuu yenye baraka'. Ni njia ya kawaida watu kuelezea sherehe zao kwa familia na marafiki.