{Picha} Rais Ruto, DP Gachagua, Raila wahudhuria misa ya kumkumbuka Jenerali Ogolla

Ibada maalum ya kumkumbuka marehemu Jenerali Francis Ogolla inaendelea jijini Nairobi.

Muhtasari

•Rais Ruto aliwasili katika hafla hiyo dakika chache kabla ya saa saba mchana akiandamana na mkewe Racheal Ruto na Naibu Rais Rigathi Gachagua.

•Katika hafla hiyo iliyoratibiwa kuanza rasmi mwendo wa saa saba mchana, maafisa wa KDF watampa heshima kiongozi wao mkuu.

Picha ya jenerali Francis Ogolla
Image: EZEKIEL AMINGA

Ibada maalum ya kumkumbuka marehemu Jenerali Francis Ogolla inaendelea jijini Nairobi.

Hafla hiyo inafanyika katika uwanja wa Ulinzi wa michezo ulio karibu na Barabara ya Langata. Inangozwa na makasisi kutoka jeshi.

Rais William Ruto, naibu wake Rigathi Gachagua, waziri mkuu wa zamani Raila Odinga, viongozi wengine wakuu wa serikali na familia ya marehemu Ogolla ni miongoni mwa wageni wengine waliohudhuria hafla hiyo.

Rais Ruto aliwasili katika hafla hiyo dakika chache kabla ya saa saba mchana akiandamana na mkewe Racheal Ruto na Naibu Rais Rigathi Gachagua.

akiwasili kwenye misa ya wafu ya marehemu Ogolla mnamo Aprili 19, 2024.
Raila Odinga akiwasili kwenye misa ya wafu ya marehemu Ogolla mnamo Aprili 19, 2024.
Image: EZEKIEL AMINGA

Kiongozi wa ODM Raila Odinga alikuwa amefika muda mfupi kabla yao.

Katika hafla hiyo iliyoratibiwa kuanza rasmi mwendo wa saa saba mchana, maafisa wa KDF watampa heshima kiongozi wao mkuu.

Kando na saluti ya bunduki 19, Ogolla pia ataonyeshwa heshima kwa utulivu na ukimya wa dakika moja na muundo wa mtu aliyetoweka.

Taarifa kutoka kwa Waziri wa Ulinzi Aden Duale ilisema kwamba wengine wanaotarajiwa katika hafla hiyo ni pamoja na maafisa wakuu wa serikali, viongozi wa Bunge, mahakama, viongozi wa kisiasa, makamanda wa sekta ya usalama na wanadiplomasia.

"Heshima hizo zitajumuisha ibada ya kanisa, gwaride la kijeshi na salamu ya bunduki 19," Duale alisema katika taarifa.

Mwili wa marehemu Ogolla uliondoka Mashujaa Funeral Home kwenda Ulinzi Sports Complex mwendo wa saa tano unusu asubuhi.

Sherehe hiyo itaanza rasmi mwendo wa saa saba mchana ikianza kwa maombi, ikifuatiwa na hotuba na hatimaye heshima za kijeshi.

Ruto pia alitangaza siku tatu za asubuhi kitaifa kwa heshima ya Ogolla.

akimsalimia waziri Kindiki Kithure baada ya kuwasili kwenye misa ya wafu ya marehemu Ogolla mnamo Aprili 19, 2024.
Naibu rais Rigathi Gachagua akimsalimia waziri Kindiki Kithure baada ya kuwasili kwenye misa ya wafu ya marehemu Ogolla mnamo Aprili 19, 2024.
Image: EZEKIEL AMINGA
awasili kwenye misa ya wafu ya marehemu Ogolla mnamo Aprili 19, 2024.
Kinara wa ODM Raila Odinga awasili kwenye misa ya wafu ya marehemu Ogolla mnamo Aprili 19, 2024.
Image: EZEKIEL AMINGA
akizungumza na waziri Aden Duale baada ya kuwasili kwenye misa ya wafu ya marehemu Ogolla mnamo Aprili 19, 2024.
Naibu rais Rigathi Gachagua akizungumza na waziri Aden Duale baada ya kuwasili kwenye misa ya wafu ya marehemu Ogolla mnamo Aprili 19, 2024.
Image: EZEKIEL AMINGA
baada ya kuwasili kwenye misa ya wafu ya marehemu Ogolla mnamo Aprili 19, 2024.
Waziri Kindiki Kithure baada ya kuwasili kwenye misa ya wafu ya marehemu Ogolla mnamo Aprili 19, 2024.
Image: EZEKIEL AMINGA
Picha ya jenerali Francis Ogolla
Image: EZEKIEL AMINGA
wakati wa ibada ya kumkumbuka marehemu Ogolla
Viongozi wakati wa ibada ya kumkumbuka marehemu Ogolla
Image: EZEKIEL AMINGA
wazidikisha mwili wa marehemu Ogolla
Wanajeshi wazidikisha mwili wa marehemu Ogolla
Image: EZEKIEL AMINGA