Tazama nyuso na maelezo ya wanajeshi waliouawa kwenye ajali ya ndege ya Alhamisi

Ndani ya ndege hiyo walikuwepo maafisa waliojitolea maisha yao kwa huduma, ujasiri na wajibu.

Muhtasari

•Walikuwa ni wapenzi wa mtu, wazazi, watoto au rafiki; kila mmoja na hadithi yake ya kipekee na ndoto.

Yeye ni fundi wa ndege na alikuwa miongoni mwa wapiga picha rasmi katika Jeshi la Kenya Airforce, waliokuwa wakifanya kazi na Mkuu wa Majeshi.
Sajenti Rose Nyawira. Yeye ni fundi wa ndege na alikuwa miongoni mwa wapiga picha rasmi katika Jeshi la Kenya Airforce, waliokuwa wakifanya kazi na Mkuu wa Majeshi.
Image: HISANI

Mkasa wa ajali ya ndege ya kijeshi iliyotokea Alhamisi katika eneo la Elgeyo Marakwet umeacha huzuni kubwa kwa jamii ya wanajeshi, na kuacha familia na marafiki wakiomboleza.

Ndani ya ndege hiyo walikuwepo maafisa waliojitolea maisha yao kwa huduma, ujasiri na wajibu.

Walikuwa ni wapenzi wa mtu, wazazi, watoto au rafiki; kila mmoja na hadithi yake ya kipekee na ndoto.

Katika kuheshimu maisha na taaluma ya kijeshi ya mashujaa hawa walioaga dunia, Rais William Ruto alitangaza kipindi cha siku tatu cha maombolezo kuanzia Ijumaa, Aprili 19, 2024.

Katika kipindi hichi, bendera ya Kenya, ile ya KDF na EAC itapepea nusu mlingoti nchini na misheni za Kenya nje ya nchi.

Hizi hapa nyuso za wanajeshi walioaga;

Brigedia Swale Saidi. Alikuwa kutoka Jeshi la Kenya na alikuwa ameandamana na Mkuu wa Majeshi katika misheni.
Brigedia Swale Saidi. Alikuwa kutoka Jeshi la Kenya na alikuwa ameandamana na Mkuu wa Majeshi katika misheni.
Image: HISANI
Meja George Benson Magondu. Alikuwa rubani katika chopa hiyo iliyoanguka.
Meja George Benson Magondu. Alikuwa rubani katika chopa hiyo iliyoanguka.
Image: HISANI
Image: HISANI
Kapteni Hillary Litali. Alikuwa mmoja wa marubani katika chopa hiyo.
Kapteni Hillary Litali. Alikuwa mmoja wa marubani katika chopa hiyo.
Image: HISANI
Sajenti Cliphonce Omondi. Alikuwa afisa wa Kenya Airforce.
Sajenti Cliphonce Omondi. Alikuwa afisa wa Kenya Airforce.
Image: HISANI
Kanali Duncan Keitany. Alikuwa mwalimu wa ndege na ardhi katika Jeshi la Kenya Airforce
Kanali Duncan Keitany. Alikuwa mwalimu wa ndege na ardhi katika Jeshi la Kenya Airforce
Image: HISANI
Sajenti Mkuu John Kinyua Mureithi. Alikuwa fundi wa ndege.
Sajenti Mkuu John Kinyua Mureithi. Alikuwa fundi wa ndege.
Image: HISANI