Mkenya afungwa jela Marekani baada ya kumbaka ajuza

Muhtasari

• Mkenya mmoja kwa jina la Samuel Wambugu amehukumiwa kifungo jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mama mzee huko Marekani.

• Wambugu ambaye alikuwa mfanyikazi wa The Heritage of Overland Park nursing home huko Marekani alipatikana na hatia ya kumbaka ajuza mmoja mwenye alikuwa ametafuta hifadhi huko. Wambugu alihukumiwa kifungu katika gereza la Johnson County Januari 26 kwa kosa la kujilazimisha kwa ajuza wa miaka 86.

Samwel Wambugu
Image: FOX4

Mkenya mmoja kwa jina la Samuel Wambugu amehukumiwa kifungo jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mama mzee huko Marekani.

Wambugu ambaye alikuwa mfanyikazi wa The Heritage of Overland Park nursing home huko Marekani alipatikana na hatia ya kumbaka ajuza mmoja mwenye alikuwa ametafuta hifadhi huko. Wambugu alihukumiwa kifungu katika gereza la Johnson County Januari 26 kwa kosa la kujilazimisha kwa ajuza wa miaka 86.

Heritage of Overland Park Nursing Home
Image: Facebook

Akizungumzia unyama alioupitia ajuza huyo, mkurugenzi wa mpito katika kituo cha Kansas Advocates for Better Care, Mitzi McFatrich alisema, “Kufikiria kuhusu mwanamke mzee ambaye inasadikika hakuwa na uwezo wa kujilinda alipokuwa akitendewa ukatili wa kingono kwa kweli ni jambo la kuvunja moyo sana.”

Katika Habari kutoka kituo hicho zilizowekwa wazi na shirika la Habari la FOX4, Kituo hicho kilidhibitisha kisa hicho na kusema kwamba mara baada ya kupata Habari za ukatili huo, walitoa taarifa kwa vyombo vya kisheria vilivyochukua hatua Madhubuti.

Kituo hicho cha Heritage of Overland Park kilianzishwa miaka kumi 10 iliyopita ili kutunza watu wenye shida za akili na kushirikiana na familia ili kuwapa wakaazi wa kituo hicho hali bora ya Maisha iwezekanavyo.