'Sitawaangusha,'Martha Karua azungumza baada ya kutajwa kuwa mgombea mwenza wa Raila

Muhtasari
  • Martha Karua azungumza baada ya kutajwa kuwa mgombea mwenza wa Raila
Kutoka kushoto gavana wa Kitui Charity Ngilu,Munya,Martha Karua na mwakilishi wa wanawake Sabina Chege
Image: ENOS TECHE

Uchaguzi wa Agosti 9, ni wakati wa wanawake wa Kenya kuchukua uongozi wa nchi, kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua amesema.

Maoni yake yalikuja muda mfupi baada ya kiongozi wa ODM Raila Odinga kumtangaza kama naibu mgombea urais wa muungano wa Azimio. Katika hotuba yake ya kukubalika, Karua alikaribisha uteuzi huo akibainisha kuwa hatua hiyo ni ushindi mkubwa kwa wanawake wa Kenya.

"Huu ni wakati kwa wanawake wa Kenya. Ni wakati rafiki yangu Marehemu Wangari Maathai angejivunia. Huu ni wakati wa kutuingiza zaidi katika uongozi wa Kitaifa na kaunti."

Kiongozi wa Narc Kenya alienda mbali zaidi na kutoa shukrani zake kwa kuteuliwa kuwa mgombea mwenza.

Alielezea kujitolea kufanya kazi na Raila katika kuwasilisha Kenya yenye ustawi. "Nimefurahishwa sana kwa uamuzi wa kuteuliwa kuwa Naibu Rais mgombea wa Muungano wa Azimio. Ni safari ya kibinafsi lakini pia ya kitaifa."

"Ni Azimio pekee inayoweza kuwapeleka watu wa Kenya mbele. Tunakuomba uje kufanya kazi nasi sitawaangusha."