Mama Ngina,Rais Uhuru wawasili Uhuru Gardens kwa sikukuu za Madaraka

Muhtasari
  • Mama Ngina,Rais Uhuru wawasili Uhuru Gardens kwa sikukuu za Madaraka
Image: ENOS TECHE

Mke wa rais wa Kenya Mama Ngina Kenyatta na mwanawe Uhuru Kenyatta wamefika katika bustani ya Uhuru kwa sherehe za siku ya Madaraka.

Mama Ngina alifika dakika 30 kabla ya Uhuru aliyeingia akiandamana na mkewe Margaret Kenyatta.

Akiwa amevalia blauzi na sketi ya Ankara ya rangi ya hudhurungi, Mama Ngina alijifunika kichwani alipokuwa akielekea kwenye jukwaa la watu mashuhuri.

Kwa upande mwingine, msafara wa Rais Uhuru Kenyatta uliondoka Ikulu hadi Uhuru Gardens mwendo wa 10:45am na kuwasili saa 11:15 asubuhi.

Uhuru aliwapungia mkono Wakenya kwenye sherehe huku msafara wake ukimfuatilia kwa karibu. Alipunga mkono huku 'Kenya taifa, nchi yetu' ikiimbwa kwa nyuma.

Uhuru alipokelewa na naibu wake William Ruto katika bustani ya Uhuru.

Hapo awali, Ruto alielekea uwanjani akiandamana na Rachel Ruto. Urembo na mavazi ya kizalendo ndiyo yalikuwa utaratibu wa siku kwa wageni walioketi kwenye jukwaa.

Wageni wengine ambao wamewasili ni pamoja na Rais wa Seirra Leone, Safaricom na mwenyekiti wa KQ Michael Joseph, mwenyekiti wa EACC Eliud Wabukala.