Orodha ya IEBC ya Uteuzi wa Vyama vya Siasa

Chama cha Jubilee kilimteua dadake mkubwa wa Uhuru Kristina Wambui kwenye Seneti.

Muhtasari

•Majina hayo yaliwasisilishwa na vyama vikuu vya kisiasa vya hapa nchini  kwa ajili ya uteuzi katika mabunge yote mawili.

•Vyama vinavyoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta, Naibu Rais William Ruto, na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga viliteua washirika wa karibu na maafisa wakuu wa chama.

akizungumza katika kikao kilichopita.
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati akizungumza katika kikao kilichopita.
Image: MAKTABA

Tume ya uchaguzi na mipaka nchini (IEBC0 ilitoa kijitabu cha orodha za uteuzi wa vyama vya siasa ambacho kilisambazwa kote nchini.

Katika kijitabu hicho ambacho kilikuwa na majina zaidi ya 10,000, maelezo yalijitokeza kuhusu majina makubwa ambayo yamependekezwa kwa uteuzi.

Hii hapa link ya orodha ya uteuzi wa vyama vya siasa:-

Majina hayo yaliwasisilishwa na vyama vikuu vya siasa vya hapa nchini  kwa ajili ya uteuzi katika mabunge yote mawili.

Vyama vinavyoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta, Naibu Rais William Ruto, na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga viliteua washirika wa karibu na maafisa wakuu wa chama.

Chama cha Jubilee kilimteua dadake mkubwa rais Uhuru Kristina Wambui kwenye Seneti.

Katika orodha ya chama iliyochapishwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, Kristina ameorodheshwa wa pili kati ya wanawake 16 ambao chama tawala kimewasilisha kama wateule wake katika bunge hilo.

Kristina, 70, anayejulikana pia kama Kristina Pratt, hana historia ya kisiasa ya hapo awali licha ya kutoka kwa moja ya familia kuu za kisiasa nchini Kenya.

Wanawake wengine mashuhuri waliopendekezwa pamoja na Kristina ni Seneta wa Uasin Gishu Margaret Kamar, 63, na Ann Kananu ambaye ni gavana wa sasa wa Nairobi.

Chama cha Raila cha ODM kwa upande wake kimewasilisha majina ya Mbunge wa Suba Kusini na kiongozi wa Wachache John Mbadi, Irene Mayaka, Seneta Mteule Rosa Nyamunga na Mbunge wa Busia mwanamke Florence Mutua katika Bunge la Kitaifa.

Chama hicho pia kinanuia kuwazawadia vijana wawili ambao ni watetezi wake wakali, Fikirini Katoi Kahindi na Hezena Lemaletian kwa kuwakabidhi viti katika Seneti.

Kahindi alifukuzwa Chuo Kikuu cha Maasai Mara na baadaye Chuo Kikuu cha Pwani ambako alikuwa kiongozi wa wanafunzi. Amekuwa mpigania haki.

Majina mashuhuri katika orodha ya Ruto katika Bunge la Kitaifa la UDA ni pamoja na Mwakilishi wa Wanawake wa Laikipia Cate Waruguru na Mbunge wa Starehe Charles Njagua almaarufu Jaguar.