Msiamini kile mnasoma mitandaoni kunihusu-DP Gachagua kwa wakosoaji wake

Akizungumza akiwa mjini Mombasa, Gachagua alisema yuko tayari kufanya kazi na viongozi wote.

Muhtasari
  • Naibu Rais Rigathi Gachagua amemjibu Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuhusu mjadala unaoendelea kuhusu kutolipwa kwa ushuru
Image: Twitter

Naibu Rais Rigathi Gachagua amewataka viongozi wa kisiasa kote katika mirengo ya kisiasa nchini kufanya kazi pamoja.

Akizungumza akiwa mjini Mombasa, Gachagua alisema yuko tayari kufanya kazi na viongozi wote.

“Mimi ni mtu rahisi sana wale ambao hawapo pamoja nasi msiamini mnachosoma kwenye mitandao ya kijamii kunihusu, nimetoka mbali hadi sasa ambapo Mungu ameniweka, mimi ni mtu mnyenyekevu sana unaweza  njoo ofisini kwangu wakati wowote tunapozungumza. Ninasikiliza kwa makini na kuheshimu maoni ya kila mtu," DP Gachua alisema.

Gachagua aliwahakikishia wabunge hao utumishi wake kwa nchi akisema hilo ni jukumu lake kuu.

"Rais na mimi tayari tumewasomesha watoto wetu. Kwa hivyo hatuna kazi nyingine ya kufanya isipokuwa kuwatumikia watu wa Kenya," alieleza.

Naibu Rais Rigathi Gachagua amemjibu Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuhusu mjadala unaoendelea kuhusu kutolipwa kwa ushuru.

Bila kutaja jina la Uhuru, Gachagua alisema hakuna kurudi nyuma katika azimio la kuhakikisha wale wasiolipa ushuru wanafanya hivyo.

"Ata ukipiga kelele, hata ukienda wapi, kodi utalipa," Alizungumza Gachagua.