Mwili wa mwanamume aliyetoweka siku kadhaa wapatikana umeoza nyumbani kwake

Mwanamume huyo wa umri wa miaka 40 aliripotiwa kutoweka wiki moja iliyopita.

Muhtasari

• Mwanamume huyo alipatikana akining'inia kutoka kwa paa la nyumba yake mtaani Kayole.

crime scene
crime scene

Mwili wa mwanamume wa miaka 40 aliyeripotiwa kutoweka kwa Zaidi ya wiki moja iliyopita umepatikana ukiwa umeoza katika nyumba yake mtaani Kayole, Nairobi.

Mwanamume huyo aliripotiwa kutoweka mnamo Februari 25 na mwili wake ulikuja kupatikana katika nyumba yake ukiwa umening’iniwa kutoka kwenye paa la nyumba yake, Kamba shingoni.

Kulingana na polisi waliofika kwenye eneo la tukio, walisema mwili wa mwanamume huyo ulikuwa umeanza kuanza vibaya ukibubujikwa na harufu mbaya, na walikisia kwamba huenda alijitoa uhai siku ambayo aliripotiwa kutoonekana na marafiki zake.

Polisi ambao waliuchukua mwili huo na kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri kufanyiwa uchunguzi, walisema chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana.

Visa vya watu kujitoa uhai haswa katika kaunti ya Nairobi katika siku za hivi karibuni vimekuwa vikiripotiwa, huku wadadisi wakisema huenda wengi wanajitoa uhai au kunyongwa kwa njia tatanishi.

Kwa wale wanaojitoa uhai, wadadisi wanahisi kwamab ni kutokana na msongo wa mawazo ambayo aghalabu yanasababishwa na gharama ya juu ya maisha kipindi hiki ambapo thamani ya shilingi ya Kenya dhidi ya dola ya Kimarekani inazidi kudorora na kuporomoka kwa kasi kubwa.

Tukio hili linajiri wakati ambapo polisi wameanzisha uchunguzi kubaini kifo cha mgonjwa aliyesemekana kujirusha kutoka kwa wadi ya ghorofa ya saba katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta katika kile kimezua mseto wa maoni iwapo ni kujitoa mhanga au ni kurushwa na mtu alaiyekuwa na nia mbaya na yeye.

Watu wanahimizwa kuchukua hatua za mapema kutafuta huduma za ushauri nasaha kuhusu afya ya akili, tatizo ambalo limetajwa kuwaathiri wakenya wengi ambao hawajui kama wanatatizwa na tatizo hilo.