Nangoja DCI wachapishe picha za waliovamia mali ya Kenyatta-Donald Kipkorir asema

Kilichowashangaza Wakenya wengi ni kutokuwepo kwa polisi wakati shamba la Kenyatta liliposhambuliwa.

Muhtasari
  • Kipkorir sasa anasema kama vile wiki jana, polisi wanapaswa kutuma picha za wale waliovamia mali ya Uhuru.
Wakili Donald Kipkorir na rais Uhuru Kenyatta
Wakili Donald Kipkorir na rais Uhuru Kenyatta
Image: State House Kenya (Facebook), Donald Kipkorir (Twitter)

Wakenya wengi bado wanashutumu maandamano ambayo yameshuhudia majambazi wakishambulia shamba la aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta.

Kilichowashangaza Wakenya wengi ni kutokuwepo kwa polisi wakati shamba la Kenyatta liliposhambuliwa.

Wakili Donald Kipkorir ambaye amekuwa mshirika wa muda mrefu wa Raila na Uhuru amelaani kitendo hicho.

Kipkorir sasa anasema kama vile wiki jana, polisi wanapaswa kutuma picha za wale waliovamia mali ya Uhuru.

Baadhi ya wafuasi wa Azimio wameikashifu serikali kwa kupanga shambulizi katika shamba la Uhuru.

Watu hao walivamia shamba na kuanza kukata miti. Mara walipomaliza kukata miti, baadhi ya watu walianza kuiba mbuzi na kondoo waliofugwa katika shamba la Kenyatta.

"Na subiri @NPSOfficial_KE & @DCI_Kenya kuweka picha za magaidi waliovamia na kuiba mali ya Uhuru Kenyatta kutoka Northlands!"

Kipkorir sasa anataka polisi kuchapisha picha za wahuni waliomvamia Uhuru.

“Jana, IG wa Polisi Koome aliahidi Fire and Brimstone kwa wale ambao watavunja sheria leo. Leo wahuni wamevamia mali ya Kenyatta Northlands na kuondoka na wanyama wa bei ya juu. Wakenya wanasubiri Polisi na DCI kuchapisha picha za magaidi hao,” Kipkorir amesema.