Dorcas Rigathi asema anamwombea naibu rais

Alidai kuwa anamwombea sana Nibu Rais Rigathi Gachagua

Muhtasari

•Aliongeza kuwa DP aliweza tu kuwa vile alivyo kupitia maombi. Dorcas alionyesha upendo wake kwa DP, na kujitolea kusimama pamoja naye

MUHUBIRI DORCAS RIGATHI
Image: DORCAS RIGATHI/FACEBOOK

Mke wa naibu rais Rigathi Gachagua,Dorcas Rigathi amekanusha wakosoaji wanaotilia shaka maombi yake kwa mumewe Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Katika video iliyoonekana na gazeti la Star, Dorcas alisema Gachagua hangefikia msimamo wake ikiwa hangeombewa.

"Hakuna mwanaume ninayemuombea bora zaidi ya huyo mtu (Gachagua)... Kwa hivyo, ambaye amekuwa akiniomba nimuombee zaidi, naweza kukuambia anaombewa, na analindwa," alisema.

Aliongeza kuwa DP aliweza tu kuwa vile alivyo kupitia maombi. Dorcas alionyesha upendo wake kwa DP, na kujitolea kusimama pamoja naye na kwamba ana  uhakika kuwa watafanya uamuzi ulio sawa.

"Ninampenda mtu huyo na ninasimama naye; ninamuombea na nina uhakika sana atafanya maamuzi sahihi," aliongeza.

Gachagua na Mchungaji Dorcas wameoana kwa miaka 35.