Rigathress;Mkewe naibu rais,apewa jina la matani

Wakenya kwenye mtandao wa twitter wamempa jina mke wa naibu wa rais.

Muhtasari

Mke wa naibu rais katika mkutano wiki uliopita katika chuo kikuu cha Nairobi,aliomba kupewa jina la matani linalolingana na la Riggy G.

MUHUBIRI DORCAS RIGATHI
Image: DORCAS RIGATHI/FACEBOOK

Dorcas Gachagua,mke wake naibu rais Rigathi Gachagua sasa amepewa jina lake la utani,Rigathress ,na Wakenya kwenye mtandao wa twitter.

Hili linakuja baada ya Pastor Dorcas kuomba kupewa jina la matani linalolingana na lile alilopewa naibu rais almaarufu Riggy G.

Jina la matani laki lake naibu rais'Riggy G' alilopewa na Ivy Chelimo lilienea mno na hata sasa limejulikana nchini kote.Viongozi wakiwemo Rais William Ruto mara kwa mara katika mikutano hata wametumia jina hilo la Riggy G.

Mke wa naibu rais katika mkutano wiki uliopita katika chuo kikuu cha Nairobi,aliomba kupewa jina la matani linalolingana na la Riggy G.