46 wakamatwa wakati wa maandamano ya Azimio - Kindiki

Alisema washukiwa kumi na wanne walikamatwa ndani ya Nairobi huku 32 wakinaswa katika maeneo tofauti ya mkoa wa Nyanza.

Muhtasari
  • Raila alikuwa ametoa wito wa kurejelewa kwa maandamano makubwa siku ya Jumanne ili kuendelea kuzidisha shinikizo kwa serikali kuhusu lalama za uchaguzi na gharama ya maisha.
KITHURE KINDIKI AKIWA MBELE YA KAMATI YA USAILI YA BUNGE LA KITAIFA
Image: EZEKIEL AMINGA

Takriban watu 46 walitiwa mbaroni siku ya Jumanne wakati polisi walipokuwa wakifanya kazi kote nchini kudhibiti maandamano ya Azimio yaliyoitishwa na kiongozi Raila Odinga.

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki alisema katika taarifa kuwa 46 hao wanashukiwa kupanga wizi, uchomaji na uharibifu wa mali.

“Washukiwa wote watafikishwa mahakamani kesho,” Kindiki alisema.

Alisema washukiwa kumi na wanne walikamatwa ndani ya Nairobi huku 32 wakinaswa katika maeneo tofauti ya mkoa wa Nyanza.

Waziri huyo pia alisema uchunguzi unaendelea ili kuwakamata washukiwa wengine kuhusiana na machafuko yaliyoshuhudiwa Jumanne.

Raila alikuwa ametoa wito wa kurejelewa kwa maandamano makubwa siku ya Jumanne ili kuendelea kuzidisha shinikizo kwa serikali kuhusu lalama za uchaguzi na gharama ya maisha.

Polisi, hata hivyo, walichukua hatua kimkakati na kuwazuia waandamanaji kufikia , cbd na kukabiliana na hatua hiyo kuwa pigo.

Taarifa za usalama za viongozi wa Azimio akiwemo Raila na Kalonzo Musyoka pia ziliondolewa.

Hii ilitanguliwa na matukio ya pekee katika baadhi ya maeneo ya jiji ambapo basi lilichomwa moto na magauni kwenye Barabara ya Ngong na lori lililokuwa likisafirisha chuma kutoka Mombasa hadi Kampala kuteketezwa kwenye barabara ya Southern bypass.

Zaidi ya hayo, machafuko yalishuhudiwa Eastleigh ambapo kituo cha mafuta cha Juja Shell kilishambuliwa na kuporwa mitungi 12 ya gesi.

Aidha vingozi wa Azimio walimshutumu naibu rais Gachagua na waziri Moses KUria kwa madai kwamba waliwaajhuni ili wavuruge maandamano.

Pia muungano huo ulisema kwamba utarejelea maandamano siku ya Alhamisi.